Pages

Pages

Pages

Saturday 20 June 2015

UTAFITI WAONYESHA KWAMBA WATOTO WAONGO NI WEREVU!


Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.

Watafiti katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa nyuma ya meza zao.
Wale waliodanganya kuhusu kile walichofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.
Mmoja ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uwongo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment