Pages

Pages

Pages

Tuesday 2 June 2015

KUNDI LA AL SHABAAB LATEKA VIJIJI KENYA

Wapiganaji wa Al Shabaab
Hofu kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kundi la wapiganaji wa Al Shabaab limeviteka vijiji kadhaa katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo hilo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment