Pages

Pages

Pages

Wednesday 6 May 2015

WAJUMBE HALMASHAURI KUU CCM WAFUNGA OFISI YA KATIBU WILAYA

Na Hastin Liumba, TaboraZAIDI ya wajumbe 130 wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tabora mjini wameweka kufuli na kufunga ofisi ya katibu wa chama hicho Bakar Lwasa wakimtuhumu tuhuma mbalimbali ikiwemo upotevu wa sh milioni nane (8).

Wajumbe hao baada ya kufunga ofisi hiyo waliandamana hadi kwa katibu wa CCM mkoa Janeth Kayanda wakiwa na mabango mbalimbali yaliyokuwa na ujumbe wa Bakar Lwasa kuondoka.
Baadhi ya mabango hayo yalisomeka hivi ‘Bakar hatukutaki’,Nenda kwenu Kaliua,Toka Bakar toka’.
Akisoma risala mbele ya katibu wa CCM mkoa Deus Malugu alisema katibu wa wilaya Tabora mjini amekigawa chama kwa muda mrefu na anashiriki njamaza kuchafua baadhi ya viongozi.
Deues aliendelea kusoma risala yake na kudai katibu huyo ameshiriki upotevu wa kiasi ch sh milioni 8 za kata ya Gongoni na kuanzisha matawi mawili ya CCM Mdoe na CCM Bachu.
Aidha tuhuma nyingine ni tuhuma nyingine ni mwezi April 4,2015 aliwapa sh 50,000 makatibu kata wawili Oscar Matasi kata ya Ntalikwa na Rose Kilimba kata ya Itonjanda ili wawe mashahidi kuwa mjumbe wa mkutano mkuu taifa Emmanuel Mwakasaka ameanza kampeni za ubunge jimbo la Tabora mjini.
Aidha risala hiyo pia ilieleza katibu huyo aliwaomba endapo watakubali mpango huo ipo sh milioni moja (1,000,000) ambayo watagawana Sh 500,000 kila mmoja endapo wataivisha dili hiyo.
Aidha msoma risala huyo alisema katibu wa CCM wilaya Bakar Lwasa amejigamba hakuna wa kumuhamisha na ametumwa na uongozi wa CCM taifa kwa kazi maalumu hivyo yeye ni Super Star.
Alisema kufuatia mgogoro huo kudumu muda mrefu mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi na katibu mkuu wa CCM taifa Abdulrahaman Kinana walihaidi kuingilia kati lakini kutokana na kukosekana majibu leo hii wamefunga ofisi ya katibu huyo hadi hapo aakapohamishwa.
Aidha wajumbe hao wametoa muda wa siku tatu majibu yapatikane na kama sivyo wataachia nyadhifa zao zote na kumuachia ofisi katibu Lwasa anedelee na majigambo yake.
Wajumbe hao kwa nyakati tofauti kupitia risala hiyo wamesema katibu huyo ameleta madhara makubwa ikiwemo ujenzi wa ofisi za CCM kata kusimama,umoja wa wanaCCM Tabora kuparanganyika na CCM Tabora kuwa ngome yetu.
Naye katibu kata wa Ntalikwa Oscar Matasi alikiri kupewa fedha kiasi cha sh 50,000 ili kushiriki kutunga uongo fedha ambazo aliziwasilisha kwa katibu wa mkoa Janeth Kayanda kama ushahidi.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alijibu taarifa hizo anazo ili hajaona kama wajumbe hao wameandamana kwenda CCM mkoa.
"Mimi ninazo taarifa hizo……lakini sijaona wajumbe hao kuandamana kama ulivyoona wewe na kufungwa ofisi sina taarifa," alisema.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Janeth Kayanda alipokea risala hiyo na kuhaidi malalamiko hayo atayafikisha CCM Taifa kwa hatua zaidi.
Kayanda alisema Bakar Lwasa CCM mkoa inaendelea kumshikilia hadi hapo uongozi wa juu CCM Taifa utakapotoa maelekezo na napokea risala yenu na Funguo tatu za kufuli mililofunga ofisi ya atibu huyo.

No comments:

Post a Comment