Pages

Pages

Pages

Wednesday 6 May 2015

WAAFGHAN 4 KUNYONGWA KWA MAUAJI


Waandamanaji wakipinga mauaji ya Farkhunda
Jaji wa Mahakama ya Afghan amewahukumu wanaume wanne adhabu ya kifo kwa muua kwa kumshambulia mwanamke mmoja mjini Kabul zaidi mwezi mmoja uliopita.

Mwanamke huyo anayeitwa Farkhunda alipigwa hadi kufa na kundi la watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kimakosa kuchoma kitabu cha Koran.
Mwili wake ulichomwa mwoto. Watu wengine 49 wanaendelea na kesi, wakiwemo polisi 19 wanaotuhumiwa kwa kushindwa kuingilia kati kumwokoa mwanamke huyo.
Mauaji hayo yalisababisha hasira kutoka maeneo mbali mbali duniani ambayo pia yalisababisha maandamano nchini Afghanistan kupinga jinsi mwanamke huyo alivyotendewa.
CREDIT: BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment