Pages

Pages

Pages

Monday 25 May 2015

UELEWA MDOGO CHANZO WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA MAJUMBANI

Na Hastin Liumba, Nzega 
UELEWA mdogo kwa kinamama wajawazito na  waliojifungua bado ni tatizo linalosababisha wajawazito wengi kujifungulia majumbani na kushindwa kuhudhuria kliniki.


Mganga mfawidhi wa zahanati ya Mwanhala wilaya ya Nzega mkoani Tabora Daniel Maguta alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari.

Maguta alitoa ufafanuzi huo kufuatia ujumbe wa shirika la EGPAF linalofadhiliwa na mashirika ya CDC na USAID nchini Marekani ukiongozwa na afisa habari na mawasiliano Anna Sawaki kutembelea zahanati hiyo.

Alisema hali hiyo imekuwa ikipelekea wajawazito hao kujifungulia nyumbani hali ambayo inahatarisha maisha ya mtoto anayezaliwa endapo mama atakuwa na maambukizi ya VVU.

Alisema katika kipindi cha mwezi januari hadi april mwaka huu jumla kinamama 260 waliokuwa wakihudhuria kliniki ni 103 tu walijifungulia zahanati na 157 walijifungulia hospitali jirani na wengine nyumbani.


Alisema hali hiyo imepelekea wao kutenga muda na kuwatembelea wajawaito majumbani na kuwapa elimu ya kuhudhuria na kujifungulia Zahanati kwani watapata huduma za uhakika.


Aidha alibainisha kati ya wajawazito 260 waliohudhuria kliniki wajawazito 19 waligundulika wana maambukizi ya VVU ana tayari walianza tiba na hali zao zinaendelea vizuri.

Akizungumzia changamoto Maguta alisema wanakabiliwa na uhaba wa watumishi kwenye zanahati hiyo kwani wapo watatu tu huku kata hiyo ikiwa na wakazi 25,438 wanaopata huduma za afya katika zahanati hiyo.

Aidha alitaja myingine ni uhaba wa dawa za SP kwa wajawazito,vifaa tiba na upungufu wa dawa.

Aidha alisema bado kuna wajawazito ambao wanahudhuria kliniki wakiwa wamechelewa kwani wengi wao hufika wakiwa wamebakiza miezi michache wajifungue.

No comments:

Post a Comment