Pages

Pages

Pages

Monday 25 May 2015

MWILI WA MWANAMAPINDUZI THOMAS SANKARA KUFUKULIWA LEO HII

Hayati Thomas Sankara
Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unakisiwa kuwa wa rais wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.

Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake.
Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987.
Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka 1983.
Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou.
Mjane wa Sankara, Mariam
Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Familia yake inashuku kuwa huenda mwili huo sio wake.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment