Pages

Pages

Pages

Saturday 9 May 2015

MUBARAK NA WANAWE WAFUNGWA MIAKA MITATU JELA

Hosni Mubarak na wanawe wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
Mahakama ya uhalifu ya Misri imetoa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu, kwa rais wa zamani, Hosni Mubarak, na watoto wake wawili wa kiume,kutokana na kesi ya rushwa iliokuwa ikiwakabili.

Mwaka jana, wote watatu walipatikana na hatia ya kutumia fedha za taifa, kukarabati nyumba za familia yao.
Lakini mahakama ya rufaa ilifuta kesi hiyo na kutaka kesi ifanywe tena.
Bwana Mubarak alipatikana hana makosa, katika kesi zote nyengine, pamoja na kuamrisha mauaji ya waandamanaji, katika mwamko wa Januari mwaka 2011, ambao ulimaliza utawala wake wa miaka 30.
Washtakiwa hao watatu huenda wasitumikie kifungo kwa sababu ya muda waliokaa kizuizini.
(Wana siku 60 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.)
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment