Pages

Pages

Pages

Saturday 30 May 2015

MAREKANI KUFANYA UCHUNGUZI WA KIMETA

Bakteria wa Kimeta
Idara ya ulinzi nchini Marekani imeamrisha kufanyika uchunguzi mkubwa kuhusu jinsi mahabara zake zinashughulikia kimeta, baada ya kufichua kuwa jeshi lake lilituma kimakosa sampuli za bakteria ya kimeta zilizo hai, kwenda vituo vya utafiti nchini marekani na pia nchi za ng'ambo.

Makao makuu ya ulinzi nchini Marekani Pentagon, yanasema kuwa mahabara kwenye majimbo 11 nchini marekani pamoja na nchini Korea kusini na Australia sasa zinafahamika kupokea sampuni za kimeta ambayo ni bakteria hatari.
Pentagon inasema kuwa bado hakujaripotiwa madhara yoyote kutoka na visa hivyo lakini imetaka utafiti wowote unaofanyiwa sampuli hizo kusitishwa.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment