Pages

Pages

Pages

Friday 8 May 2015

DAVID CAMERON AONGOZA KWA KURA UINGEREZA

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron anaongoza kwa kura
Waziri mkuu David Cameron anaelekea kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Uingereza hiyo jana.

Chama chake cha Conservative kimejiongezea hadi sasa jumla ya viti 20 na kusajili ushindi katika majimbo 279.
Chama kikuu cha upinzani Chama cha Leba kimesajili jumla ya viti 217 hii ikiwa na viti 25 chini ya idadi iliyokuwa nayo katika bunge lililopita
Huku matokeo ya theluthi moja ya maaneo bunge yakiwa yametangazwa waziri mkuu David Cameron anaonekana kurejea afisini lakini bila idadi kubwa ya wabunge ikimaanisha kuwa Chama cha Conservative kitalazimika kuunda serikali ya muungano.
Cameron amesema kuwa anapania kuendelea kuiongoza uingereza ya pamoja .
Shirika La BBC linakisia kuwa Cameron na Chama chake huenda wakasajili ushindi wa maeneo bunge 329.
Waziri huyo mkuu hata hivyo anawaomba wafuasi wake wasubiri hadi matokeo kamili yatangazwe
Waziri huyo mkuu hata hivyo anawaomba wafuasi wake wasubiri hadi matokeo kamili yatangazwe.
Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland kutoka kwa chama cha kitaifa cha Scotland National Party SNP .
Licha ya Matokeo hayo Mazuri huko Scotland ambapo SNP ilisajili ushindi mkubwa wa majimbo 50 chama hicho hakikutamba katika maeneo ya England na Wales.
Chama cha The Liberal Democrats wanaelekea kusajili matokeo duni wakiwa tayari wameshinda viti vinane pekee.
Nyota wa chama hicho (Lib Dems) Vince Cable, Ed Davey na Danny Alexander wote wameshindwa katika uchaguzi huo.
BBC ilikuwa imebashiri kuwa Conservative watasajili ushindi katika maeneo bunge 329, Labour 233, the Lib Dems 8, SNP 56, Plaid Cymru 3, UKIP2, Greens 1 na vyama vyengine vidogo viti 19.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment