Pages

Pages

Pages

Saturday 9 May 2015

BONDIA STANLEY MABESI 'NINJA' AMFAGILIA KOCHA SUPER D

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa katika picha na pamoja na bondia wa zamani Stanley Mabesi 'Ninja' wa pili kushoto  ambaye kwa sasa anaishi nchini Holland mji wa amsterdam wengine ni mashabiki wa mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa  pamoja na bondia wa zamani Stanley Mabesi 'Ninja' ambaye kwa sasa anaishi nchini Holland katika mji wa Amsterdam. Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa siku nyingi Stanley Mabesi 'Ninja' aliyekuwa akizipiga kuanzia mwaka 1985 na kumalizia mpambano wake wa mwisho mwaka 2001 na kujijengea heshima kubwa nchini juu ya mchezo wa masumbwi amempongeza kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' alipokuja hivi karibuni akitokea nchini Holland anakoishi.
Mabesi alimpongeza Super D kwa kuwainua vijana mbalimbali katika mchezo wa masumbwi mojawapo ni kuwapa vifaa vya mchezo huo bure au hata kuwapatia kwa gharama nafuu zaidi vifaa hivyo na kubuni njia mojawapo rahisi kwa kuwaandalia DVD zenye mafunzo ya mchezo huo huku akichanganya na mabondia mbalimbali wa nje wanaotamba duniani.


Mapambano hayo aliyocheza kwa nyakati tofauti yalikuwa ya kusisimua zaidi katika kipindi chake wakati mchezo huo ukiwa na mashabiki wengi lakini kwa sasa umekosa wafadhili wanaojitokea kudhamini, tofauti na nchi za wenzetu.

No comments:

Post a Comment