Pages

Pages

Pages

Saturday 18 April 2015

WASHUKIWA WA UGAIDI WAKAMATWA AUSTRALIA

Mshukiwa wa ugaidi nchini Australia
Polisi katika jimbo la Victoria nchini Australia wanasema kuwa wamewakamata wanaume watano kufuatia oparesheni kubwa ya kupambana na ugaidi kwenye mji wa Melbourne.

Wawili kati ya wanaume hao walio na umri wa miaka 18 walikamatwa baada ya kushukiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi yaikiwemo ya kuwalenga polisi.
Mshukiwa mwingine naye alikamatwa kufuatia sababu zinazohusiana na silaha. Shughuli za kuwatafuta washukiwa wengine zinaendelea sehemu zingine za mji wa Melbourne.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment