Pages

Pages

Pages

Wednesday 8 April 2015

NYALANDU: UJANGILI BADO NI TATIZO KUBWA.

Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema ujangili ni suala la watu wachache wenye roho mbaya wanaotaka utajiri wa haraka wakishirikiana na watu waliopo kwenye mtandao ndani na nje ya nchi ili kupata masoko.

 
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati akihojiwa katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV.
 
Alisema ulinzi wa wanyamapori, misitu na mazao ya misitu na mali kale ni changamoto kubwa kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka siku hadi siku na ardhi ikiwa ni ile ile.
 
Alisema haiwezekani Waziri au viongozi wa kisiasa wenyewe waweze kukabiliana na ujangili na ndiyo maana wameongeza nguvu kazi yenye mafunzo thaibiti na vitendea kazi vya kisasa.
 
“Tumeongeza idadi ya askari wanyamapori, mfumo wa utendaji kazi na vitendea kazi, magari na kutengeneza mifumo ya utawala ikiwamo kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori kwa kuwa na kikosi cha kupambana na ujangili uliokithiri,” alisema.
 
Alisema serikali inalitazama suala la ujangili kama ni tatizo linaloendelea na kwamba kuna juhudi zinazoonekana na zisizoonekana zinazofanywa.
 
Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kuwa na tembo wengi na ya pili Afrika kwa kuwa na wanyamapori wengine.
 
Alisema siyo lazima kuchoma meno ya Tembo kwani kuna meno makubwa mbayo yanatoweka na miaka ya baadaye yatakuwa ni kivutio kwa watu mbalimbali na kwamba yanaondolewa katika soko kwa ajili ya kuyahifadhi kwa uwazi baada ya kuwepo kwa makubalino ya mifumo ya kikompyuta yenye kutambua meno hayo.
 
Nyalandu alisema ushirikiano wa Watanzania na vyombo vya ulinzi na usalama, ndiyo wa kukomesha vitendo hivyo ili kupunguza matukio ya ujangili.
 
Alisema zaidi ya asilimia 70 ya watalii wanaofika nchini wanakuja kuona wanyamapori na kupanda mlima Kilimanjaro na ndiyo maana serikali imeiimarisha ulinzi wa wanyamapori.
 
Alisema serikali iko katika mpango wa kushirikiana na wadau wa ndani na nje kwa kuifanya Tanzania iendelee kuheshimika kwa ulinzi wa wanyamapori kama tembo na kwamba wako mbioni kutoa sensa ya tembo na faru waliopo nchini.
 
Alisema mfumo wa kuwezesha kuwahesabu wanyama hao umekamilika kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) na mashirika ya Marekani na Ujerumani kwa kutengeneza mfumo wa kuhesabu wanyama na kwamba ndani ya kipindi kifupi serikali itaeleza hali halisi ikoje.
 
“Tumefanikiwa kuishawishi jamii ya kimataifa kuwa changamoto zilizopo zimedhibitiwa na Tanzania ilishatangaza kuachana na uuzaji wa meno ya tembo nje ya nchi, na tumefanya hivyo ili kupambana na mpango wa ongezeko la mahitaji katika masoko nchini China na kwingine, tunawalinda kwa kudhibiti masoko yanayozidi kuongezeka na kupandisha bei ya nyara,” alibainisha. Umuhimu wa wananchi kushiriki kutoa maoni katika miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge kwenye mkutano wa 19 unaoendelea mjini Dodoma.
 
Naye Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ameandikiwa barua na wadau hao wakimuomba atumie nafasi yake kama msemaji mkuu wa kambi hiyo bungeni kuishauri serikali iwasilishe miswada hiyo chini ya mfumo wa kawaida na siyo chini ya hati ya dharura kwani unawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni yao kwenye miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge.
 
Tangu serikali iseme kuwa inakusudia kuwasilisha miswada hiyo chini ya hati ya dharura, wadau wa habari wamekuwa wakiomba ibadili msimamo kwani kufanya hivyo kutawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni juu ya miswada hiyo kabla ya kuwa sheria.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment