Pages

Pages

Pages

Thursday 2 April 2015

MASOMO YA SAYANSI YAONGEZA UFAULU KIDATO CHA 4

Shule ya sekondari ya wavulana Tabora


Na Hastin Liumba, Nzega
Ufaulu kwa wanafunzi wa kidado cha nne wilayani Nzega mkoani Tabora umeongezeka mpaka kufikia asilimia 72 ongezeko la asilimia 9 ukilinganisha na asilimia 63 kwa mwaka 2013.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Abrahaman Mdeme alisema kuwa masomo hayo ya sayansi yameongeza ufaulu wilayani hapo mpaka kushika nafasi ya 46 kitaifa ambapo mwaka mwaka 2013 wilaya hiyo ilishika nafasi ya 74.

Mdeme alisema masomo ya sayansi  kwa vitendo wanafunzi wameyapenda kutokana na kufanya kazi wanayoina moja kwa moja tofauti na hapo awali.

Alisema kuwa wilaya imeshika nafasi ya tatu kimkoa ambapo nafasi ya kwanza imechukuliwa na wilaya ya Igunga huku ya pili ikichukuliwa na Tabora Mjini ambapo ya nne (4) ikichukuliwa na Urambo huku Kaliuwa ikishika nafasi ya Tano Sikonge ikishika nafasi ya sita wakati wilaya ya Uyui ikishika nafasi ya saba.

Alisema kuwa wilaya ya Nzega itahakikisha inaendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali ya kimkoa na kitaifa ilikupandisha elimu wilayani hapa.

Kuhusu vyumba vya maabara vinavyofanya kazi kikamilifu ni vyumba 47 huku vyumba 70 vikiwa katika hatua mbalimbali za matengenezo ya ukamilishaji wakati mahataji halisi ya wilaya yakiwa ni vyumba 117.

Afisa Elimu sekondari  wilaya Chatta luleka alisema kuwa mafanikio hayo yamepatikana kutokana na baadhi ya wazazi kushirikiana na waalimu ikiwa na kuchangia chakula cha mchana.

Alisema awari wazazi walikuwa hawana mwamuko wa Eilimu na kusababisha elimu kushuka wilayani hapa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa na shuguli za mashambani.

Alisema kuwa juhudi za waalimu zimeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na waalimu wengi kujitoa kusaidia wanafunzi na kuongeza kuwa mahusiano mazuri yameongezeka.

Luleka alisema kuwa Ofisi ya mkuu wa wilaya imekuwa ikifuatilia kwanyakati mbalimbali maendeleo ya waalimu na wanafuzi kwa ujumla hali iliyotilia mkazo zaidi kupanda kwa kiwango cha Elimu wilayani hapa.

Alisema kuwa ongezeko la vitabu vya sayansi vimesaidia wanafunzi kujisomea zaidi kwanyakati mbalimbali hali inayosababisha wanafunzi wengi kupenda masomo hayo.

Akiungumzia changamoto zinazoikabili Idara hiyo nipamoja na upungufu wa Idadi ya waalimu wa sayansi hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi kukosa waalimu wa sayansi hata hivyo jitihada za kupata waalim bado
zinaendelea.

No comments:

Post a Comment