Pages

Pages

Pages

Thursday 9 April 2015

KAYA 945,000 KUFIKIWA NA TASAF III

 
Na Hastin Liumba, Kigoma
JUMLA ya Kaya 945,000 kati ya milioni moja zinatarajiwa kufikiwa na kutambuliwa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF) katika awamu ya tatu mwaka 2015.



Mkurugenzi wa TASAF nchini Ladislaus Mwamanga alisema hayo wakati akiongea na wahasibu, waratibu, maafisa wafatiliaji, waratibu wa mikoa,menejimenti ya TASAF na waandishi wa habari toka mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi.
Mwamanga alisema lengo la kufikiwa kwa kaya hizo ni malengo ya TASAF awamu ya tatu ikiwa na kutambua Kaya zinazoishi katika umasikini kuwanusuru ngazi za Vijiji na Mitaa.

Alisema kazi za TASAF awamu ya tatu itafanya kazi zake katika kipindi cha miaka kumi kwa awamu mbili za miaka mitano mitano.

Alisema kabla ya kuanza kutekelezwa kwa TASAF awamu hii elimu itatolewa ambapo makusudio awamu hii kulenga sekta tatu za Maji, Afya na Elimu.
Mkurugenzi huyo anabainisha zaidi kuwa kama TASAF, wameangalia zaidi utekelezaji ambao unalenga kuwajengea zaidi uwezo watu hasa walengwa ambao ni Kaya masikini zaidi.
Aidha Mwamanga alibainisha hadi sasa kwa awamu hii inakuja na malengo ya kuwa na miradi ambayo inatokana na Uhawilishaji wa fedha kati TASAF na Kaya walengwa.
Alisema kutokana na hilo hadi sasa kama TASAF walishafanya utafiti wakutosha kwa baadhi ya Halmashauri hapa nchini na matokeo yake ni mazuri.
Alisema malengo ya hili wanataka kila Halmashauri nchini zifikiwe kwa hili kila kaya masikini zaidi zenye mlo mmoja kwa siku.
Alisema katika Uhawilishaji fedha watatoa fedha kwakaya hizo ili waunde vikundi baadaye vya kuweka akiba na kujikwamua na lindi na umasikini.
Hata hivyo mkurugenzi huyo alitoa taarifa ya upotoshaji kwa baadhi ya watu kuwa TASAF imebadilika inatoa fedha siyo sahihi.

Alisema ukweli ni kwamba hatutoi fedha bali tunahawilisha fedha na siyo tunagawa fedha.

No comments:

Post a Comment