Pages

Pages

Pages

Saturday 4 April 2015

JAMII YAASWA KUTHAMINI WATOTO WENYE ULEMAVU


Na Hastin Liumba, TaboraJAMII imeaswa kubadili mitizamo potofu waliyonayo dhidi ya watoto wenye ulemavu wa viungo au Albino na kuwathamini kama watoto wengine kwa kuwa Mungu amewapa uwezo na vipaji mbalimbali.



Ni jukumu la kila mzazi, mlezi, familia au jamii kwa ujumla kuwathamini na kufichua mtu yeyote anayeendekeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto hao wenye ulemavu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Kudra Mwinyimvua aliyewakilishwa na Afisa Ustawi wa Jamii wa mkoa Baraka Makona katika kilele cha warsha ya Baraza la Watoto Wenye Ulemavu.

Alisema serikali inaziagiza familia zote zenye watoto wenye ulemavu na jamii kwa ujumla kuwathamini kama wanavyothamini watoto wengine wasio na ulemavu na kuwapa haki zao za msingi pasipo kuwabagua vinginevyo wazazi au familia husika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 ‘Ni wajibu wa kila halmashauri, taasisi zote za serikali, watu binafsi na jamii kwa ujuma kubadilika na kukemea mitizamo yote iliyo potofu dhidi ya watoto hawa na kukataa aina zote za udhalilishaji dhidi yao’.

Alisema ili kutokomeza vitendo vya mauaji kwa watu wenye albinism, Makona alitoa wito kwa jamii kuwafichua bila hofu watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kikatili ili waweze kufikishwa mbele ya sheria.

Aidha aliziagiza mamlaka zote za serikali na watu binafsi kuweka utaratibu mzuri wa kurekebisha miundombinu yao na kujenga majengo yaliyo rafiki kwa watu wote wenye ulemavu kwa mujibu wa Sheria Na. 9 ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2009.

Aidha alibainisha ili kuboresha huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu kwa kila halmashauri hususani suala la elimu na afya, takribani Maofisa Ustawi wa Jamii 28 wameajiriwa katika mkoa mzima na kuongeza kuwa halmashauri zote zimeagizwa kuendelea kutenga fedha ili kupunguza kero zinazowakabili.

Askofu Isaya Ilumba wa kanisa la Free Pentekoste (FPCT) jimbo la Tabora ambaye ndiye msimamizi mkuu wa shule ya watoto wenye ulemavu ya Furaha alieleza kanisa linajitahidi kuwahudumia watoto hao changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni uhaba wa fedha kwa ajili ya mahitaji yao ya chakula, matibabu.

No comments:

Post a Comment