Pages

Pages

Pages

Thursday 9 April 2015

HAKUNA FEDHA ZA FREEMASON WALA UCHAGUZI-TASAF

Na Hastin Liumba, Kigoma
UONGOZI wa mfuko wa Maendeleo ya jamii Tanzania (TASAF) umesema utekelezaji wa kazi za mfuko huo kwa awamu ya tatu hakuna mahusiano yoyote ya fedha za Freemason, mikopo wala kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015.



Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa TASAF, mwezeshaji Zuhura Mdungi alisema kuna upotoshaji mkubwa katika jamii wa namna ya utekelezaji wa mfuko kwa awamu hii.

Mdundi akitoa mada kwenye kikao cha kazi mkoani Kigoma kilichoshirikisha waandishi wa habari,waratibu,wahasibu na maafisa wafuatiliaji alisema dhana hiyo inapaswa kusemewa ili kazi zilizopangwa kunusuru Kaya masikini inafanikiwa.

Alisema kama TASAF safari hii wamejipanga kufanyia kazi mapungufu yaliyojiri katika awamu zilizopita ili kusiwepo na upotoshaji wa namna yoyote.

Mdungi alisema suala la Uhawilishaji fedha limefanyiwa kazi ili kuona fedha zinazotolewa zinalingana na hali halisi ya maisha ya sasa katika Kaya.

Hata alisema pamoja na kujipanga katika kutoa taarifa sahihi kwa jamii bado kuna changamoto kwani usomaji wa taarifa za TASAF ni tatizo wapo wasomaji wetu hawana miwani (hawajui kusoma wala kuandika).

Alisema TASAF waliliona hilo na wamelifanyia kazi na sasa wametengeneza utaratibu wa kuwa na Maigizo,sikukuu za kitaifa,Ngonjera na taarifa nyingine kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha alisema TASAF imejipanga vyema kushirikisha jamii katika utoaji taarifa sahihi ili kusiwepo na upotoshaji wowote ule.

Mwezeshaji huyo alisema lengo la TASAF kwa awamu hii ni kuona lengo la kunusuru Kaya masikini linafanikiwa.

No comments:

Post a Comment