Pages

Pages

Pages

Tuesday 7 April 2015

CHUO CHA UALIMU NYAMWEZI TABORA KUPUNGUZA UHABA WA WALIMU

Displaying 3.jpg
Mkurugenzi wa chuo cha Musoma utalii na chuo  kipya cha ualimu Nyamwezi Shaban Mrutu.
Displaying IMG-20150406-WA0007.jpg
Displaying IMG-20150406-WA0008.jpg
Majengo mpya ya chuo kipya cha ualimu Nyamwezi yanavyoonekana kwa mbele. (Picha zote na Hastin Liumba,)

Na Hastin Liumba,Tabora

CHUO cha Ualimu Nyamwezi kilicho chini ya chuo cha Musoma Utalii mkoani Tabora kimenzishwa na matarajio yake makubwa ni kupunguza ukubwa wa tatizo la uhaba wa walimu wenye sifa.

Hatua hii inaonyesha dhhiri kuwasasa uwepo wa tatizo hili utakuwa ni ndoto kwani hata Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeridhi na tayari namba za usajili ili huduma hiyo iwepo imetolewa rasmi mwaka 2015.

Shaban Mrutu ni Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii tawi la Tabora kilipo chuo hicho, alifanya mahojiano na mwandishi na kuelezea mikakati,malengo na changamoto zake  pindi chuo kitakapoanza mafunzo.

Mrutu anabainisha malengo ya kufungua chuo hicho yanaedana na hali halisi ya upungufu na uhaba wa walimu na utoaji wa ajira mpya uliopo hivyo wana mategemeo makubwa kuondoa tatizo hilo.

Mkurugenzi huyo alisema chuo cha ualimu Nyamwezi kilisajiliwa kutoa elimu ya ualimu ngazi ya Stashahada kupitia wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kikiwa na nanba za usajili za (CU.148) na wana matarajio ya kufikiwa kwa utoaji wa cheti ngazi ya Shahada.

Alisema kwa sasa chuo kinajipanga kuanza kutoa elimu hiyo mwezi Juni 2015 na vijana watakaochukuliwa ni wale ambao wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi itakuwa imeweka vigezo na muongozo wake pia Chuo hiki kiko Kata ya Ipuli manispaa Tabora.

Alisema hadi sasa kama chuo wameanza kupokea maombi na wanatarajia kuanza na wanafunzi wapatao 150 kwa wakati mmoja.

Mrutu alisema chuo kitapokea wanafunzi wa bweni na kutwa hasa ikizingatia chuo kina Hostel za kutosha wanafunzi hao kuishi na kuendelea na masomo yao.

Alisema wanachuo watakaosoma ni wale waliomaliza kidato cha nne na sita huku wengine wakiwa ni wale waalimu wa shule za msingi ambao watakuwa na  elimu ngazi cheti watahitaji kusoma na kupata cheti ngazi ya Stashahada.

Alisema kwa wale waaalimu ambao wapo ndani ya manispaa watapata fursa nzuri ya kusoma bila kutoka katika vituo vyao vya kazi walivyoajiriwa.

Kupanua soko la ajira
Mrutu anasema ana imani kuwa licha kulenga kupunguza uhaba wa walimu mkoani Tabora na mikoa ya jirani pia anaongeza nafasi za ajira kupitia chuo ambapo jumla ya watumishi na walimu wakufunzi 16 wataajiriwa.

Anasema utoaji wa elimu katika chuo hicho ana matumaini makubwa kwamba elimu ni kuelimisha na kuelimisha ni suala la lazima siyo la hiari ili kufikia malemgo yake.

Alisema suala la kuelimisha ni sawa na sayansi ya kuumba mtu ili mtu naye aumbe huduma na vitu na atoe huduma pamoja kutatua changamoto zake ili uwekezaji makini kwenye elimu unaohitajika uwepo.

Alisema katika uwekezaji makini uwepo mipango mikakati inahitajika zaidi sanjari na kutumia maarifa ya wengi kutengeneza njia sahihi zitakazotuvusha kuelekea Elimu iliyojikita kwenye Sayansi na Teknolojia.

Kuelimisha kutoa elimu kwa watu kunatokea pale hatua za kivitendo zinaposhabihiana na maneno ya wafanya maamuzi ili fikra mpya zisichukue nafasi ya kufanya na kutenda kazi za mazoea na kushindwa kufikia malengo ya chuo cha Ualimu Nyamwezi

Alisema haya anayasema ili kuweka wazi ni jinsi gani wameamua kwa dhati kuanzisha chuo hicho ili kitoe huduma tarajiwa kwa walengwa ambao ni Malimu wenye sifa ili watoto watakaopikwa darasani wawe bora.

Changamoto zilizopo kwa sasa.Mrutu anabainisha changamoto kabla ya kuanza kutoa huduma zake ni wapo wanafunzi ambao tayari wameanza kuleta maombi lakini wizara ya elimu na  mafunzo  ya ufundi imechelewa kutoa vigezo na masharti ya kuanza kupokea wanafunzi na walimu wa shule za msingi.

Aidha changamoto nyingine ni mfumuko wa bei vyakula na vitu kwa wanachuo wa bweni na kutwa kwani fomu ikishatolewa mwanafunzi atakaporipoti anakuta kuna bei za vitu zimebadilika na kupanda na hivyo chuo hulazimika kuingia gharama isiyolingana na fomu inavyoeleza bei za awali.

Alisema changamoto nyingine ni gharama za kupanda kwa bei za vitabu kwani chuo kina Maktaba yake lakini kumekuwa na upungufu wa vitabu kadhaa na serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa shule za serikali pekee na siyo taasisi binafsi.

Mazingira ya chuo
Mrutu anasema mazingira ya chuo yako vizuri kwa wanafunzi kujisomea kwa utulivu na kuna vyumba vya kutosha na viwanja vya michezo.

Aidha alisema kuhusiana na suala la Ada mkurugenzi huyo alisema chuo gharama zake zimeangalia zaidi hali za maisha kwa sasa na kwamba ni nafuu huku mzazi/mlezi akilipa Ada hiyo mara mbili mihula miwili tofauti.

Malengo ya chuo cha ualimu Nyamwezi.
Mkurugenzi Mrutu anabainisha malengo ya chuo hicho na kusema wanatarajia kuendelea kuboresha mindombinu yate muhimu ya chuo ili kuweza kufikia malengo na kuchukua wanafunzi watakaofikia 400 kwa wakati mmoja.

Aidha kingine alisema ni kuongeza vifaa na watumishi wenye sifa ili chuo kiweze kuwa na sifa ya utoaji huduma stahiki kwa wanachuo ili kufikia malengo ya utoaji wa cheti ngazi ya Shahada mkoani Tabora.

Alisema wataendelea kadri siku zinavyosonga mbele kuboresha huduma ya elimu bora tofauti na huduma ya vyuo vingine hali ambayo itawawezesha wahitimu wake kuwa na maadili ya ualimu pamoja na moyo wa kujitolea.

Alisema elimu ya sasa wamejipanga kutoa wahitimu kuendana na hali ya sasa ya Sayansi na Teknolojia ya Dunia sanjari na ushindani uliopo wa soko la Ajira la Afrika Mashariki.

Mrutu anasema wa menza kujipanga vyema kuanza ujenzi wa shule ya Msingi chuoni hapo ili waalimu, wahitimu na wanafunzi kufanya mazoezi shuleni hapo hali ambayo itawajengea uwezo walimu hao.

Miradi ya chuo.Anasema chuo kwa sasa ina mipango ya kuanzisha miradi ya mashamba,ufugaji mifugo mbalimbali na kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kujipatia fedha zitakazosidia kuendesha mahitaji mengine kama mafuta ya magari na chakula kwa walimu na wanachuo.

hastinliumba@gmail.com-0788-390788

No comments:

Post a Comment