Pages

Pages

Pages

Tuesday 24 March 2015

KILUVYA BINGWA SDL, HIYOOOOO DARAJA LA KWANZA

kiluvya united
Timu ya Kiluvya United ya mkoa wa Pwani jana imetawazwa Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya kuifunga Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.


Kiluvya United inaunganana timu za Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma, Mbao FC ya Mwanza na Mji Njombe ya Njombe kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL)msimu ujao, huku timu za Ujenzi Rukwa, Katavi FC na Volcano zikishuka daraja kutoka Ligi Daraja la Pili.

VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ianatrajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kwa wenyeji JKT Ruvu kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo timu ya Young Africans.

1 comment:

  1. safi danny kwa taarifsa za kiluvya united

    ReplyDelete