Pages

Pages

Pages

Friday 27 March 2015

BRAZIL YAICHAPA UFARANSA 3-1

Timu ya taifa ya Brazil

Brazili jana aliikimbiza mchaka mchaka Ufaransa baada ya kuichabanga magoli matatu kwa moja.

Haikuwasaidia Ufaransa kuanza kuona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli lililofungwa na Raphael Varane kwani ni kama waliichokoza kundi la nyuki kwani goli hilo lilirudishwa na Oscar dos Santos Emboaba Júnior katika dakika ya 40, na hatimaye kushindiliwa magoli mengine mawili kupitia kwa Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi hiyo inamalizika Brazil 3 Ufaransa 1.
Katika mechi nyingine za kimataifa za kirafiki zilizochezwa hapo jana, Bahrain iligeuzuwa chapati na Colombia pale waliposhindiliwa magoli 6 kwa mtungi huku Iran ikiwapa darasa Chile kwa kuichabanga magoli mawili kwa nunge.
Leo kutakuwa na mechi moja ya kimataifa ya kirafiki ambapo Canada watairibisha Guatemala.
CREDIT: BBC.

No comments:

Post a Comment