Pages

Pages

Pages

Wednesday 7 January 2015

WANANCHI WACHOMA NYUMBA TANO ZA MTUHUMIWA JAMBAZI SUGU


Na Hastin Liumba,Igunga
WANANCHI wa kata ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, wameyakimbia makazi yao kwa ajili ya kukwepa kukamatwa na jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kuchoma nyumba tano za mtu anayedhaniwa kuwa ni jambazi.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti  baadhi ya wananchi Richard Ngilya na Amosi Makeleja walisema kuchomwa kwa nyumba hizo tano kumesababishwa na jeshi la polisi wilaya ya Igunga kuwakamata wananchi nane (8) wa kata hiyo huku wakiendelea kumlinda jambazi huyo.

Aidha Ngilya alidai kilichowashangaza wananchi ni kitendo kiilichofanywa na jeshi la polisi kwenda katika kata hiyo majira ya saa saba usiku pasipo kutaarifu uongozi uliopo na kuanza kuwakiwalazimisha wakimama kuwaonyesha waume zao ambao hawajafanya kosa la uchomaji nyumba.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwakwangu kilichopo katika kata hiyo Luhende Swala alisema askari hao waliingia katika kitongoji chake bila kumtaarifu yeye ambapo waliwakamata baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho na kuondoka nao.

Aliendelea kusema baada ya kubebwa wananchi hao ndipo wananchi walishikwa na hasira na kujikusanya na kwenda kuchoma nyumba tatu za Matembe  ambazo jambazi huyo alikuwa amewajengea ndugu zake huku idadi ya nyumba zilizochomwa zikifika tano hadi sasa.

Aliongeza  baada ya kuchomwa nyumba hizo tatu kundi la wananchi hao lilielekea katika nyumba za baba yake na jambazi huyo kwa ajili ya kwenda kuzichoma lakini muda mfupi polisi wa kituo kidogo Igurubi walifika na kuanza kufyatua risasi za moto zilizasaidia kuwatawanya wananchi

Naye Mtendaji wa kata ya igurubi Mdeka Said alibainisha kuchomwa kwa nyumba hizo kumetokana na baadhi ya wananchi kukamatwa na polisi kufuatia tukio la kuchomwa nyumba za jambazi huyo mwishoni mwa mwaka 2014 aliongeza hadi sasa ni nyumba tano zilizochomwa huku akifafanua nyumba mbili za bati na tatu za matembe ambapo hakutajwa thamani ya nyumba zote.

Mtendaji huyo alitaja majina ya wananchi walikamatwa Mbeshi Reuben, Shija Jilala, Ng’ombe Igoye, Masesa Pamba, Martin Charles, Lushuminkono Maige, Emmanuel Mwizamhindi, Mwandu Shusha alisema kitendo cha kukamatwa wananchi hao kimeleta mtafaruku mkubwa katika kata ya Igurubi.

Diwani wa kata ya Igurubi Bw, Edson Sadani alikiri kukamatwa kwa wananchi wake na kusema kuwa kitendo kilichofanywa na polisi sio cha kiungwana kwa kuwa hawakushirikisha uongozi wowote hata walipomaliza kuwakamata wananchi wake.

Akijibu tuhuma hizo Mahona Malendeja akiwa kituo cha polisi Igunga huku akivinjari bila mashaka alisema yeye sio jambazi wala hajawahi kupatikana na shitaka lolote linalohusu ujambazi.

Alisema kilichosababisha nyumba zake kuchomwa moto ni sababu ya kumwonea wivu wa kibiashara aliongeza kuwa yeye amekuwa mfanyabiashara mkubwa anayeuza mafuta ya petrol, diesel ikiwa ni pamoja na kununua ngozi.

Kwa upande kamanda wa polisi kamishna msaidizi mkoa wa Tabora (ACP) Suzana Kaganda alidai kuwa yuko likizo hivyo hawezi kuzungumzia kitu chochote naomba umpigie kamanda aliyepo mimi nipo likizo.

No comments:

Post a Comment