Pages

Pages

Pages

Thursday 1 January 2015

MAJUU HAMNAZO: MWANAMKE MWENYE ASHKI MAJINUNI ALALA NA WANAUME 140 NA KUWEKA ORODHA YA VIWANGO



Sandy Nardo, 53, kutoka Dublin, Scotland anawapima wanaume waliooa, mapenzi ya mtungo na hata mumewe wa zamani kwa viwango vya mapenzi tangu alipopoteza bikira yake akiwa na miaka 19 kwa mwanamuziki wa Kitaliano.

Mwanamke huyo mwenye ashki majinuni amekwishafanya ngono na wanaume 140 na amekuwa akiwaorodhesha kwenye kadi maalum pembeni ya kitanda chake kina anapomaliza kuibanjua amri ya sita.
Sandy anawalinganisha katika makundi mbalimbali 'hali ya mahaba, ngono au upigaji wa busu, mtazamo, umalizaji na muda anaotumia'.
Bi Nardo, kutoka jijini Dublin, alisoma shule ya Kikatoliki yenye msimamo mkali na akapoteza bikira yake kwa Luciano, 21, mwanamuziki wa Kitaliano, wakati alipokuwa akizurura jijini Milani, akiwa na miaka 19.
Miaka zaidi ya 30 baadaye tayari ana orodha ya wanaume 140 kutoka kila kona ya dunia aliofanya nao ngono wakiwemo waliooa, wapenzi wa mtungo na pamoja na mumewe ambaye aliamua kumwacha baada ya ndoa yao iliyodumu kwa miezi sita tu.
Mwanamke huyo aliyekiri kuwa na ashki majinuni alisema: "Kuna orodha ya wanaume 140 kwa hiyo itakuwa rahisi kuwasahau. Nilitaka kuwakumbuka wote - wakiwemo wale washenzi ndiyo maana nikawaorodhesha kwenye karatasi maalumu.
"Sijutii kabisa nilichokifanya. Wakati mwingine ilihitaji kutafakari lakini yote ni kumbukumbu ambayo imenifanya niwe hivi nilivyo.
"Nimezuru nchi nyingi duniani na nimelala na wanaume kutoka zaidi ya nchi 30."
Alisafiri duniani akiwa kama dansa na mkalimani, na daima aliendelea kuwaorodhesha kitabuni wanaume aliolala nao.
Wanaume wote walipewa alama chini ya kumi kutokana na ujuzi wao kitandani, muonekano wao, utajiri wao na muda wa kufanya ngono.
Pia aliwapa alama maalum kwa 'hisia zao za mahaba' - E kwa 'eucky', B kwa 'bored', Y kwa 'yum' na F kwa 'fun'.
Mwanamume pekee aliyempekecha na kumkuna ni 'Mack' - mpenzi wa muda mrefu aliyelala naye kwa miaka 20.
Chini ya orodha hiyo alikuwemo 'Mfanyakazi wa benki wa Kiingereza' aliyelala naye kwa mwaka mmoja na nusu mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambaye alimuahidi angemwacha mkewe, lakini hakufanya hivyo.
Pia alimpa alama mumewe wa zamani Rico, ambaye wakati huo alikuwa na miaka 30, waliyeoana mwaka 1985 wakati akiishi jijini Milan baada ya kuwa na urafiki wa mwaka mmoja.
Ndoa hiyo iliyokuwa na misuguano mingi ilidumu kwa miezi sita tu, lakini akafanikiwa kupata mtoto wa kiume Marco, ambaye sasa ana miaka 28, ambaye amelazimika kuridhia tabia hiyo ya mamaye katika miaka ya nyuma.
"Alikuwa na hasira na mimi kwa jinsi nilivyoyaendesha maisha yangu, lakini sasa ameamua kunikubali hivyo hivyo," alisema mwanamke huyo. "Chui hawezi kubadili madoa yake sasa kwa nini mimi nibadilike?"
Sandy alisafiri ulimwenguni kwa miongo kadhaa kabla ya kurejea nyumbani na kitabu chake kidogo chenye orodha ya wanaume hao kwa nia ya kumtunza mama yake Marie, 87, anayeumwa dementia.
"Kwa sasa natakiwa kumtunza mama yangu na nilichojaliwa ni orodha yangu ninayoipenda sana," alisema.
"Ninaposoma shajara hii, najiona kwamba nilikuwa msichana mwenye bahati sana."

No comments:

Post a Comment