Pages

Pages

Pages

Friday 2 January 2015

MAJUU HAMNAZO: MKULIMA AJENGA NYAMBIZI YAKE NA KUIWEKA MAJINI


Mkulima wa Kichina ametimiza ndoto yake ya miaka mingi ya kujijengea nyambizi inayofanya kazi.
Tan Yong, 44, kutoka mji wa Danjiangkou katika Jimbo la Hubei, daima alitamani kuona maisha yalivyo akiwa chini ya maji.

Akiunganisha vipande vya mabati na vipande vya magari mabovu, Tan aliijenga nyambizi hiyo ndani ya miezi mitano na kuiita 'Xiyangyang'.
Alisema: "Daima nimekuwa nikipenda programu za maisha ya wanyama, hususan zile zinazohusu bahari na chini ya maji.
"Sina ujuzi wowote wa uhandisi na wala sijui masuala ya kuelea au jambo kama hilo, nilijifunza mambo yote.
"Na tatizo kubwa hasa lilikuwa namna ya kuweka hewa ndani ili nisife."
Baada ya kushindwa kuizindua mwezi Agosti mwaka huu, alilazimika kurejea mezani.
Lakini akafanikiwa kuifanya ielee pamoja na kuweka umeme na akaiweka majini kwenye Ziwa NV'er ambako ilizama kwa kina cha meta 10.
"Nafahamu siyo kina kirefu kwa nyambizi, lakini inanifaa kwa sasa," alisema.
Pal Song Chia alisema: "Wanasema wanaume hawaachi kuwa vijana na Tan ni mfano halisi. Ana ndoto za ujana na sasa ameitimiza. Sijawahi kumuona akiwa na furaha kama wakati huu."

No comments:

Post a Comment