Pages

Pages

Pages

Monday 1 December 2014

WATU 10,707 HAWAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA ARUSHA VIJIJINI



Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: IMEELEZWA kuwa jumla ya watu 10,707 kutoka katika Halmashauri ya Arusha hawajui kusoma wala kuandika hali ambayo wakati mwingine inasababisha watu hao wakose huduma za msingi hasa za kijamii.
Hata hivyo, kati ya watu hao idadi kubwa ya wanawake wanaongoza katika kushindwa kujua kusoma na kuandika kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye jamii inayowazunguka.


Akiongea kwenye madhimisho ya Juma la elimu ya watu wazima lililofanyika wilayani humo mapema jana kaimu afisa elimu ya watu wazima Grace Masawe alisema kuwa bado tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika kwenye wilaya hiyo ni kubwa sana.
Masawe alisema kuwa kati ya watu 10,707  ambao hawajui kusoma kati yao wanaume ni 4,478 wakati idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake ambao ni 6,229 hali ambayo inasababisha changamoto lukuki kwenye jamii.
Alidai kuwa kutokana na halmashauri kuwa na idadi ya watu hao wasiojua kusoma wala kuandika tayari wameshaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia watu hao au kundi hilo la wasiojua kusoma wala kuandika.
"Zipo Progamu kama nane hivi ambazo sisi tunazisimama hasa kwa wale ambao ni walengwa wetu jumla zipo kama nane ambapo mpaka sasa tunaweza kujivunia faida kubwa hasa pale ambapo jamii ikiunga mkono suala hili,” aliongeza Masawe.
Awali Afisa elimu Vielezo na takwimu katika Wilaya hiyo Evarista Swai alisema kuwa kinachosababisha wanawak wengi kuongoza kwa kutojua kusoma wala kuandika ni mfumo dume ambao bado upo kwenye baadhi ya familia.
Swai alifafanua kuwamfumo dume unatokana na baaadhi ya familia kuona kuwa elimu ni maalumu kwa watoto wa kiume pekee na hivyo watoto wa kike ni maalumu kwa ajili ya kuozwa au kufanya kazi hali ambayo sasa jamii inapaswa kukaata na kipiga vita suala hilo.
“Wanawake sasa tunatakiwa kuinuka lakini kujua na kisha kutambau kuwa elimu hasa kujua kusoma na kuandika ni muhimu lakini nataka niwaambie kuwa hata wale ambao hawajui kusoma wala kuandika wasikate tamaa bali wajiunge na programu ambao zipo kwetu ili wafanikishe malengo yao hasa ya malezi bora ya familia,” aliongeza Swai.
Wakati huo huo aliwataka wale ambao hawajui kusoma wala kuandika kuachana na mila potofu kuwa elimu ni muhimu  kwa watoto hivyo basi wale ambao hawajapata wanepitwa na wakati jambo ambalo sio la kweli kwani elimu haina mwisho.

No comments:

Post a Comment