Pages

Pages

Pages

Wednesday 17 December 2014

WAIJUA CHUPA NDOGO YA 'TUSKER' WEYE?

Displaying 9.JPG
Meneja masoko wa familia ya bia ya Tusker na Pilsner, Anitha Msangi (kushoto) na Mkurugenzi wa masoko, Bw.Ephraim Mafuru katikati na Meneja ubunifu wa bidhaa zote za kampuni ya bia ya Serengeti Ms. Attu Mynah wakionyesha chupa mpya ya bia ya Tusker kwa waandishi wa habari hawapo pichani.

Displaying 5.JPG
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiwaonyesha waaandishi wa habari , hawapo pichani, mwonekano mpya ya Bia ya Tusker yenye ujazo wa mlimita 330.Displaying 6.JPG
Meneja masoko-Familia ya bia ya Tusker na Pilsner kampuni ya bia ya Serengeti, Anitha Msangi akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya uzinduzi wa chupa mpya ya Tusker yenye ujazo wa mililita 330.

Wateja wa bia ya Tusker Lager kwa mara nyingine wamepewa heshima baada ya  kampuni ya Serengeti Breweries kuingiza sokoni chupa ya bia mpya inayojulikana kama “Tusker ml330”
Chupa hii mpya imezinduliwa mapema hii leo -Golden Jubilee Tower iliyoko jijini Dar Es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Masoko wa SBL Bwana Ephraim Mafuru pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Bw. Ephraim Mafuru alisema “Mazingira ya kibiashara ya sasa yanatulazimu kufikiria zaidi ili kuhakikisha kwamba tunaambatana na uhalisia katika soko huku tukihakikisha kwamba tunamridhisha mteja wetu katika Nyanja zote”.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa familia ya Tusker na Pilsner Serengeti Breweries Ms. Anitha Msangi alisema… “Ninaamini kwamba ubunifu unainua nia na uhitaji kwa wateja. Hivyo basi matarajio yangu makubwa ni kwa wateja wetu kuipokea na kuinunua chupa hii mpya kwa wingi.” Anitha aliongeza kwamba chupa hii ya bia itapatikana na kuuzwa nchi nzima na tutahakikisha kwamba wateja wote wanaipata bila usumbufu.
Bidhaa hii mpya ina ujazo wa ml 330 na itauzwa kwa bei ya Shilingi 2,300/= kwa bei ya rejareja. Uzinduzi wa chupa hii mpya upo katika mtazamo wa kampuni wenye lengo la kwenda sambamba na hali ya soko.
Tusker ml330 imeongezeka katika idadi ya vinywaji vilivyozinduliwa na kampuni ya SBL msimu huu ikilenga kutimiza adhima ya kuingiza bidhaa mpya katika soko la Tanzania. Bidhaa hizo ni pamoja na:-Serengeti Platinum, Jebel Coconut and Serengeti Platinum ml330

Uzinduzi wa Tusker ml 330 umekuja katika msimu wa kampeni  ya Tusker FanyaKweli ambayo ina lengo la kuwahamasisha watanzania kutengeneza maisha ya baadae ambayo wote tutajivunia kwa vitendo wakati huohuo wakijifunza kupitia watu waliopata mafanikio kupitia yale waliyokuwa wakiyafanya.

No comments:

Post a Comment