Pages

Pages

Pages

Friday 12 December 2014

MUHAMMADU BUHARI KUGOMBEA URAIS NIGERIA

Muhammadu Buhari
Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria kimemchagua Muhammadu Buhari kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi Februari 2015. 

Mtawala huyo wa zamani wa kijeshi aliwashinda wagombea wengine wanne kutoka chama cha All Progressives Congress, APC -akipata kura mara tatu zaidi ya kura za mgombea aliyepata nafasi ya pili katika uchaguzi wa chama hicho.
Katika uwanja wa mpira mjini Lagos, maelfu ya wafuasi wa chama cha upinzani cha APC walipiga kura usiku kucha. Kwa kura nyingi walimchagua Muhammadu Buhari kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa rais utrakaofanyika mwezi Februari mwakani. 
Mtawala huyo wa zamani wa kijeshi atashindana na Rais aliyeko madarakani, Goodluck Jonathan, ambaye alikuwa mgombea pekee wa chama tawala cha PDP - chama ambacho kiko madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi miaka kumi na mitano iliyopita. Muhammadu Buhari alitwaa madaraka katika mapinduzi ya kijeshi miaka ya 1980. 
Utawala wake wa miezi 20 atakumbukwa kwa kampeni kali dhidi ya utovu wa nidhamu na rushwa ambayo pia iliendana na ukiukaji wa haki za binadamu. 
Baada ya kuondolewa madarakani katika mapinduzi mengine ya kijeshi, Bwana Buhari anaonekana kudhamiria kurejea madarakani kupitia njia ya uchaguzi. Uchaguzi wa mwezi Februari litakuwa jaribio lake la nne katika kuwania kiti cha urais. 
Bwana Buhari mwenye umri wa miaka 72 anaonekana ataleta upinzani mkali kwa Rais Goodluck Jonathan, endapo kwa mara ya kwanza upinzani utaungana kwa kumuunga mkono mgombea mmoja kutoka upande huo. 
Yeyote atakayeshinda atalazimika kushughulikia tatizo la kuongezeka kwa mashambulio ya kigaidi kaskazini mwa Nigeria na uchumi unaolegalega kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment