Pages

Pages

Pages

Thursday 4 December 2014

HASSAN MFAUME AIBUKA KIDEDEA KATIKA "TUTOKE NA SERENGETI"

Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya  shindano la Tutoke na Serengeti, linaloendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Bw. Hassan Mfaume ameibuka mshindi katika Shindano hilo, kulia ni Msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Abdallah Hemedy na kushoto ni Auditor kutoka Pricewater House Coopers Ltd, Golder Kamuzora hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya  shindano la “Tutoke na Serengeti” linalo endeshwa na kampuni hiyo, ambapo Hassan Mfaume ameibuka mshindi katika shindano hilo, kulia ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Abdallah Hemed. 

MKAZI WA MABIBO AIBUKA MSHINDI KWENYE MTOKO WA “TUTOKE  NA SERENGETI  ”

03rd Dec 2014, Dar es Salaam

Kampuni ya SBL leo imemzawadia Bwana: Hassan Mfaume mkazi wa Mabibo ziara ya kwenda kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti iliyolipiwa na kampuni hiyo mara baada ya kuibuka mshindi wa droo ya Tutoke na Serengeti iliyofanyika leo makao makuu ya SBL  yaliyopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Akiongea kwa njia ya simu Bwana Hassan ambaye alikua kikazi Mwanza alionekana kushangazwa na kushitushwa baada ya kusikia taarifa kwamba amekuwa mshindi. Aliishukuru kampuni ya SBL kwa kile alichokiita zawadi murua ya kipindi hiki cha sikukuu.

Hii imekuja wiki moja tu baada ya Rukia Almasi, ambaye ni Mama wa nyumbani na mkazi wa Kihonda-Morogoro kutuzwa ushindi wa Limo Bajaj katika kampeni hii inayoendelea.

Akiongea baada ya droo iliyoshuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na Bwana. Abdallah Hemedi mwakilishi wa bodi ya michezo ya bahati nasibu Tanzania, Bwana Rugambo Rodney-Meneja Chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager alisema Bwana Hassan ameshinda safari ya watu wawili iliyolipiwa gharama zote ikimaanisha kwamba anaruhusiwa kwenda na mwenza wake na SBL watagharamia kila kitu kuanzia malazi, usafiri pamoja na vivutio mbalimbali.

Rodney aliwasihi watanzania waendelee kushiriki kwani zawadi za kushindaniwa zipo nyingi. Aliongeza kwamba kampuni imelenga katika kuinua utalii wa ndani ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha sehemu ya faida kwa wateja wake baada ya mafanikio mazuri yaliyopatikana katika mwaka husika.
Kampeni ya Tutoke na Serengeti wameungana na B-Pesa wataalam wa teknolojia mpya ambao hivi karibuni wamezindua mfumo mpya wa usafirihaji wa fedha. B-Pesa watahusika pia katika kusambaza fedha kwa washindi mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi.

Ili kushinda, unachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Serengeti Premium Lager na angalia chini ya kizibo atakuta namba ambazo zinatakiwa kutumwa kwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenda namba 15317 ili kuingia katika droo.

No comments:

Post a Comment