Pages

Pages

Pages

Thursday 4 December 2014

HALMASHAURI YADAIWA KUWANYAYASA WAFANYAKAZI


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha: UONGOZI wa Halmashauri ya Arusha Mkoa wa Arusha umedaiwa kuwanyanyasa watumishi wa Idara ya Afya katika Wilaya hiyo hususani wa Hospitali ya Oltrument ambao wamejiunga na Chama cha Wafanyakazi Serikalini  (TUGHE).

Unyanyasaji huo medaiwa kuwa ni pamoja na kushindwa kuwalipa madai ya Tshs million 120 ambayo ni madai  mbali mbali ya wafanyakazi hao  toka mwaka 2009 madai ambayo watumishi katika Halmashauri nyingine nchini wamelipwa.
Wakitoa malalamiko yao kwa Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Serikali kuu na Afya  Tanzania  (TUGHE) wamedai kuwa wamechoshwa na manyanyaso na kudai kuwa wakihoji haki zao wanahamishiwa vijiji vya mbali na kueleza kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu.
Daniel Masawe ambaye ni alikuwa Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Hospitali ya Oltrument alisema kuwa, wafanyakazi katika Halmashauri hiyo wanyimwa haki zao ikiwa ni pamoja na za madai na wakiuliza, adhabu yao ni kuhamishiwa vituo vya mbali na kudai kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliopata mkasa huo.
Masawe alifafanua kuwa akiwa kiongozi alikuwa anaongoza wenzake na kufuatilia haki zao, lakini ameonekana ni mwiba ,na kudai kuwa hali hiyo ikiendelea itashusha ari ya wafanyakazi kufanya kazi na kuomba mamlaka husika kuvalia njuga suala hilo.
Naye Mratibu wa TUGHE Meru  Isack Kaserian  amedai kuwa malalamiko ya wafanyakazi ni ya msingi kuwa wamekuwa wanahoji mambo mengi ikiwa ni pamoja na mashine ya Utra-Sound inayodaiwa kuchukuliwa na kumilikiwa na mmoja wa maafisa wa Hospitali ya Oltrument lakini wanafungwa midomo.
Kimsingi alisema kitendo cha kuhamisha wafanyakazi hususani viongozi wa tawi husika la wafanyakazi ni uonevu na kudai kuwa lazima mamlaka za juu zichukue hatua na kukomesha tabia hiyo ,ikiwa ni pamoja kuendelea kuelimisha wafanyakazi haki zao ili wasimame kuwatetea .
Kwa upande wake  Katibu Mkuu TUGHE Taifa John Sanjo alisema kuwa tabia kama hiyo haiwezi kuvumiliwa na kudai kuwa akiwa kiongozi wa ngazi za juu amelivalia njuga suala hilo na kudai kuwa tayari amewasiliana na mamlaka husika kutatua na kutafuta suluhu ya matatizo hayo.
Bwana Sanjo aliwaambia wafanyakazi wa Afya waliokutana katika Hospitali ya Oltrument kuwa madai yao yatafanyiwa kazi na kuwa hawatawaonea haya waajiri wanaowanyanyasa wafanyakazi pindi wanapohoji haki zao na kudai kuwa matawi ya vyama vya wafanyakazi yamepata baraka kisheria
Alifafanua kuwa tayari walishakutana na Rais Jakaya Kikwete mapema mwaka huu wakiwa ni viongozi wa Wafanyakazi na kueleza changamoto zao ikiwa ni pamoja na tatizo la kuhamisha wafanyakazi ambao ni viongozi wa matawi ya Wafanyakazi kiholela na Rais kuonya tabia hiyo na kuagiza wasihamishwe .
Hata hivyo  Dkt Samwel Joseph ambaye ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Oltrument ,amebeza madai hayo na kudai kuwa ,hakuna fedha zozote zilizopokelewa katika Halmashauri hiyo kwa ajili ya watumishi wa afya na kueleza kuwa fedha zilizopokelewa ni madai ya watumishi wote na siyo idara ya afya .

Dkt. Joseph alisema kuwa madai ya wafanyakazi hayo bado hajaletwa kutoka  Hazina na kuwa yakiletwa watalipwa bila kikwazo .

No comments:

Post a Comment