Pages

Pages

Pages

Thursday 4 December 2014

ACHENI TABIA YA KUWATEGEMEA WAFADHILI KWENYE ELIMU - NNKO


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
MERU: IMEELEZWA kuwa tabia ya kuwategemea zaidi wafadhili kwenye mambo mbalimbali hasa ya uendeshaji wa shule ni dalili mbaya ya umaskini kwani watanzania wana uwezo mkubwa sana wa kuchangia maendeleo ya shule za binafsi na hata zile za serikali.


Kauli hiyo imetolewa na Diwani Ephata Nnko wakati akiongea na wazazi, walezi, na wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Niruvande iliopo Meru kwenye maafali yake ya kwanza yaliyofanyika jana.

Nnko alisema kuwa kwa sasa hasa katika maeneo ya vijijini bado kuna dhana kubwa ya wazazi pamoja na walezi kujikuta wakiwa wanawategemea zaidi wafadhili iliwaweze kuwasomeshea watoto wao jambo ambalo sio jema

Alidai kuwa kwa kuwategemea wafadhili hao ni ishara kuwa bado watu wa Meru lakini mkoa wa Arusha kwa ujumla hawajaweza kuthamini elimu kitu ambacho kinawezekana kama watu watajiopanga.

Alifafanua kuwa wakaati umefika sasa kwa watanzania kuweza kujiwekeza kwenye elimu na kuachana na tabia ya kuwekeza kwenye sherehe ambazo zinapita huku wengine nao wakionekana kuwategemea wafadhili bila kujua wanao toa ufadhili wakati mwingine huwa wanakwama kulingana na hali ya Nchi zao lakini hata hali ya Uchumi wa dunia.

“Inabidi sasa jamani tuweze kubadilika na tutoe kipaumbele zaidi kwenye elimu kwanini tusiweke utaratibu wa kutupia hata michango yetu kidogo kidogo kwenye elimu mbona tunaweza tu na kwenye harusi eti mbona tunachangia sana wakati chakula kinapita ila elimu haipiti hata kidogo," alihoji Nnko.

Awali mkurugenzi wa shule hiyo ambaye ni Ndewario Mbise alisema kuwa pamoja na kuwa shule hiyo ipo pembezoni mwa mji lakini wameweza kuweka mikakati mbalimbali ambayo wameigusa jamii kwa kiwango kikubwa sana.

Mbise alidai kuwa moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanasaidia watoto wenye maitaji ya msingi kama vile wanaotokea katika familia za mayatima, lakini pia hata wale ambao wanatokea katika familia ambazo hazina uwezo hata kidogo.

Alisema kuwa  mpaka sasa tayari shule hiyo imeweza kuwasaidia yatima, na wale ambao wanaotokea katika mazingira magumu wanafunzi zaidi ya 50 lengo likiwa ni kukuza zaidi elimu.

Katika hatua nyingine wahitimu hao wa darasa la saba walisema kuwa pamoja na kuwa kwa sasa kuna mikakati mbalimbali ya kuboresha elimu ambayo inatolewa na Serikali lakini kuna umuhimu  wa Serikali nayo kuweza kuangalia namna ya kushusha bei kwa vifaa mbalimbali vya shule kwani kwa wakati mwingine wanafunzi waishi vijijini wanapata shida kubwa sana ya manunuzi ya vifaa vya shule.

No comments:

Post a Comment