Pages

Pages

Pages

Monday 17 November 2014

TAZARA KINARA WA MADENI NSSF


NA JOSEPH MALEMBEKA, MOROGORO
WAKATI Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), ikikabiliwa na ukata na kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi wake, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF), umesema unaidai zaidi ya sh bilioni 10.

NSSF inadai sh bilioni 23 za michango ya wafanyakazi kwenye mashirika na kampuni mbalimbali nchini.
Hayo yalisemwa mjini hapa na Mkurugenzi wa Huduma NSSF, Crescentius Magori, katika semina ya viongozi kutoka mashamba makubwa na madogo 80 nchini yenye zaidi ya vyama 140.
“Fikiria uimara wa mfuko ulivyo, tunadai zaidi sh bilioni 23 ikiwemo Tazara zaidi ya bilioni 10, kwa wadeni wetu wanaozidi 300 huku tunazaidi ya trilioni 2 mkononi…tumeanza kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani wadeni wetu wapatao 164,” alifafanua Magori.
Katika semina hiyo, aliwasihi kuwaelimisha wakulima vijijini kujiunga na mfuko huo ili wajinusuru na changamoto ya maisha baadaye vijijini.
Magori, alisema mfuko huo sasa umefikia kutoa mafao hadi sh milioni 10.6 kwa mwezi kwa wastaafu waliokuwa wanachama.
Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliwataka watendaji hao wa kilimo mashambani, kuepusha aibu ya watumishi hewa ambao kwa takwimu za karibuni, wanaliingizia hasara ya zaidi ya sh bilioni 18 kwa mwezi.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment