Pages

Pages

Pages

Friday 28 November 2014

MSIKITI WASHAMBULIWA NCHINI NIGERIA

Taarifa kutoka mjini Kano, Kaskazini ya Nigeria, zinasema kuwa watu wengi wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu.

Ni baada ya milipuko mitatu inayoaminika kuwa ya mabomu kutokea katika msikiti ulio katikati mwa jiji karibu na eneo anakoishi Emir.
Mabomu hayo yalilipuka wakati maombi ya Ijumaa yalipokuwa yanaendelea.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, alihesabu karibu miili 50 ya waliofariki katika shambulizi hilo ingawa taarifa hizi bado hazijathibitishwa.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment