Pages

Pages

Pages

Wednesday 19 November 2014

MAKOCHA WA MPIRA WA WAVU WAPATIWA MAFUNZO


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha.
MICHEZO mingi hapa nchini inashindwa kuendelea na kufikia kiwango cha kimataifa kutokana na kutokuwepo kwa viongozi waadilifu na wanaojitoa badala yake kufanya michezo kuwa dili.



Hayo yalisemwa jana na Mdau wa michezo nchini, Deo Mtui wakati akifungua semina ya siku sita ya  makocha wa mchezo wa wavu iliyoandaliwa na Chama cha mpira wa wavu Tanzania(TAVA) inayofanyika Moshono jijini Arusha.

Alisema kuwa,tatizo lililopo katika timu nyingi za michezo ni kutokuwepo kwa viongozi waadilifu ambao wamekuwa wakiitumia michezo kama dili kwa kujipatia fedha ,kitendo ambacho kimechangia idadi kubwa ya wafadhili kupoteza imani.

Mtui alisema kuwa, endapo nchi ya Tanzania itahitaji kusonga mbele kimichezo na kuweza kucheza kimataifa ni lazima wawepo kwanza viongozi wenye mapenzi mema na michezo na waadilifu ambao wataweza kuinua michezo badala ya kuididimiza .

‘kwa kweli hali hiyo imekuwa ikiwafanya wafadhili wenye nia ya kusaidia michezo kutoendelea na ufadhili wao kutokana na kuwepo kwa viongozi ambao wamekuwa wakifanya michezo dili na kujinufaisha kupitia michezo hiyo na hivyo timu hizo kuendelea kudidimia kila siku bila mafaniko yoyote’alisema Mtui.

Naye Mwenyekiti cha Chama cha mpira wa wavu Arusha(AVA) ,Rashidi Mkanga alisema kuwa,mafunzo hayo ni muhimu sana kwa makocha hao ambao watasaidia kuinua kiwango cha michezo mkoani Arusha.

Alisema kuwa,lengo la mafunzo hayo ni kupata makocha wazuri ambao watazisaidia timu zao na hatimaye kuweza kupata timu bora ambayo itachezea mkoa na hatimaye ngazi za juu.

Mkanga alisema kuwa,wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendesha michezo hiyo ,ukosefu wa vitendea kazi vifaa vya michezo,na kuwepo kwa upungufu wa wataalamu wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment