Pages

Pages

Pages

Tuesday 4 November 2014

LIVERPOOL MDOMONI MWA MADRID

Real Madrid na Liverpool zilipocheza mzunguko wa kwanza.
Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inaingia mzunguko wa pili hii leo kwa mechi za marudiano ambapo mabingwa watetezi Real Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kukipiga na Liverpool..ambayo katika mechi ya awali ilikubali kichapo cha fedheha nyumbani Anfield.

Kocha wa Liverpool Brendan Rogers amesema hatamchezesha mshambuliaji wake Daniel Sturridge licha ya kusafiri naye hadi mjini Madrid kwa madai kuwa bado hajawa sawa kukabiliana na mechi kama hiyo.
Naye kocha wa Madrid Carlo Anceloti amesema leo anamrudisha kiwanjani Gareth Bale baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi kwa mwezi mzima. 
Kwengineko Zenit St Petersburg ya Urusi itamenyana na Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Arsenal itakuwa nyumbani Emirates wakiwakaribisha Anderletch ya Ubelgiji ilhali Juventus ya Italia wakikiputa na Olympiakos ya Ugiriki. 
Hapo kesho Manchester City watakwaruzana na CSKA Moscow ya Urusi dimbani Etihad, FC Bayern Munchen watachuana na AS Roma, wakati ambapo Ajax Amsterdam watapambana na FC Barcelona na Paris St Germain watacheza na Apoel Nicosia.
CREDIT: BBC/MICHEZO

No comments:

Post a Comment