Pages

Pages

Pages

Thursday 6 November 2014

KOMBE LA DUNIA 2022 NJIA PANDA

Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), Michel Platini
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka barani Ulaya (Uefa), Michel Platini amesema kuwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 nchini Qatar lazima zichezwe kipindi cha majira ya baridi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ufaransa amejiweka katika upinzani dhidi ya baadhi ya vilabu vikubwa vya soka barani Ulaya ambavyo vimesisitiza kuwa fainali hizo zipangwe mwezi May 2022.
Kwa kawaida fainali za Fifa za kombe la dunia huwa zinachezwa kati ya mwezi Juni na Julai, lakini Fifa imeambiwa kuwa katika majira hayo nchini Qatar kunakuwa na joto kali litakalowaweka wachezaji kwenye hatari kiafya.
Platini ameiambia BBC kuwa “haiwezi kuwa mwezi Aprili, Mei wala Juni, bali itakuwa wakati wa majira ya baridi tu,” na kuongeza kuwa mwaka 2022 michezo ya nusu fainali na fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya inaweza kusogezwa hadi mwezi Juni ikiwa ni lazima, na kwamba vilabu vinapaswa kukubali uamuzi wowote utakaokuwa umekubaliwa.
“Sio vilabu ambavyo vinacheza, ni wachezaji na sio rahisi kucheza mwezi Mei ambapo kuna joto la hadi 40c” Alisema Platini mwenye umri wa miaka 59.
Mivutano
Itakumbukwa kuwa Qatar ndiyo ilishinda haki ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo za mwaka 2022 na tangu imeshinda kumekuwa na mivutano miongoni mwa wadau mbalimbali kuhusu uwezekano wa kuchezwa nchini humo kutokana na hali ya hewa ya joto kali.
Sepp Blatter
Rais wa Fifa Sepp Baltter amekuwa akituhumiwa na baadhi ya watu kuwa ameipendelea Qatar katika mchakato huo.
Vilabu vikubwa vya ligi kuu ya England, La Liga ya Hispania na Bundesliga ya Ujerumani vinadhani kuwa mwezi Mei kutakuwa na nafuu kiasi wakati ambapo Fifa yenyewe inashikilia msimamo wa kutafuta uwezekano wa miezi ya Juni na Julai kama kawaida.
Wadau mbalimbali wenye ushawishi mkubwa katika soka duniani walikutana jumatatu mjini Zurich katika harakati za kujaribu kupata suluhu ya mgogoro huu mkubwa wa aina yake ulioiweka Fifa njia panda, na wamepanga kukutana tena mwezi Januari 2015.
Kikosi kazi kimeundwa ili kutafiti na kutoa mapendekezo yake kwa kamati ya utendaji ya Fifa mwezi Machi mwaka ujao, huku pendekezo la Fifa likiwa ni kusogeza fainali hizo hadi mwezi Novemba na Desemba 2022.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment