Pages

Pages

Pages

Wednesday 5 November 2014

BEYONCE NDIYE MWANAMUZIKI WA KIKE MWENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI

Beyonce
BrotherDanny Blog na mashirika
MWANAMUZIKI Beyonce Knowles amekuwa kinara kwa wanamuziki wa kike wanaolipwa zaidi kwa mwaka huu baada ya kukunja kitita cha Dola 115 milioni (takriban Shs. 184 bilioni).

Nyota huyo wa wimbo wa The Drunk In Love amekusanya mara mbili ya mapato ya mwaka jana baada ya kufanya ziara ya ulimwengu na kutumbuiza kwa mamilioni ya mashabiki.
Beyonce mwenye umri wa miaka 33 amepanda kutoka kwenye nafasi ya nne ya wanamuziki wanaolipwa zaidi mwaka 2013 na kumwacha kwa mbali Taylor Swift, ambaye alishika nafasi ya pili kwenye orodha ya jarida la Forbes ya wanamuziki wa kike wenye vipato vikubwa mwaka huu kwa kukusanya Dola 64 milioni (takriban Shs. 102.4 bilioni).
Taylor Swift

Beyonce pia alikusanya mamilioni kupitia kwenye ziara yake ya On The Run akiwa na mumewe Jay Z.
Albamu mpya ya Swift inayokwenda kwa jina la 1989 imeuza karibu nakala 1.3 milioni nchini Marekani katika wiki ya kwanza tu, na kuifanya albamu mpya kubwa ya kwanza katika kipindi cha miaka 12.
Mwanamuziki wa Pop, Pink (35), amepanda kutoka nafasi ya nane mwaka 2013 hadi ya tatu kwa kukusanya Dola 52 milioni (Shs. 83.2 bilioni).
Pink

"Beyonce alifanya maonyesho 95 wakati tukiendesha mchakato wetu, na kufanya wastani wa Dola 2.4 milioni (Shs. 3.84 bilioni) kwa kila mji," lilisema jarida la Forbes, likirejea taarifa kutoka jarida la Pollstar.
Mzaliwa wa Barbados, Rihanna (26), akiwa amekusanya Dola 48 milioni (Shs. 76.8 bilioni) pamoja na Katy Perry (30), aliyevuna Dola 40 milioni (Shs. 64 bilioni), wanachuana kwenye orodha ya tano bora.
Madonna (56), ambaye mwaka jana alishika nafasi ya kwanza, safari hii ameshindwa kuingia hata kwenye 10 bora.
Lady Gaga (28), amemshuka kutoka namba mbili 2013 hadi nafasi ya tisa kwa kuvuna takriban Dola 33 milioni (Shs. 52.8).
Forbes limeweka orodha hiyo baada ya kukadiria mapato kabla ya kodi kwa kutazama miezi 12 tangu Juni 2013 hadi 2014 kwa kuzingatia mauzo ya kazi, mauzo ya tiketi za matamasha, matangazo mbalimbali ya ziara na mahojiano na waandaaji wa matamasha, wanasheria na mameneja.

Orodha kamili ni hii:
1. Beyonce
2. Taylor Swift
3. Pink
4. Rihanna
5. Katy Perry
6. Jennifer Lopez
7. Miley Cyrus (wamefungana)
7. Celine Dion (wamefungana)
9. Lady Gaga
10. Britney Spears

No comments:

Post a Comment