Pages

Pages

Pages

Friday 3 October 2014

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA LAWAMANI



UBAYA WA UBALOZI WETU WA ITALY

Tunaomba uitangaze habari hii bila kuificha na wala usipunguze hata herufi moja!!!

Kila aliyewahi kuomba huduma toka ubalozi wetu wa Rome ana malalamiko yake. Ima atakuwa amecheleweshwa mno kupatiwa huduma hiyo au hakupatiwa kabisa.Muda mrefu tumenyamaza kimya tukitegemea kuwa hali ingebadilika, lakini kila siku zinavyokwenda mambo ndivyo yanavyozidi kuwa magumu na kuharibika hasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kutozingatiwa matatizo yetu limekuwa ni jambo la kawaida mno kiasi cha kutufanya tujiulize mara mbili.. Sisi kweli ni raia wa Tanzania wenye haki ya kupatiwa msaada toka ubalozini kwetu?

Mara zote msaada tunaokuwa tukiuhitaji SI PESA, kiasi cha kwamba Mh. Balozi aseme kuwa nchi yetu haina uwezo wa kipesa kusaidia raia wake. Msaada tunaoomba ni KUPATIWA VYETI HUSIKA ILI NASI TUWEZE KUKAMILISHA HATI ZA UHALALI WA UKAAZI WETU.

Matatizo yetu yana sehemu tatu kuu zifuatazo:
  1. Hivi sasa watu wengi pasi zetu zinaisha 2015 na tumeshamuomba Mh.Balozi amtume Afisa wa pasi-japo kwa gharama zetu - aje kututatulia tatizo hilo HAJAFANYA LOLOTE. Mh.huyo katuimbisha kuwa angemtuma Afisa wa pasi August au September, kuja kuonana nasi na miezi hiyo imeshapita na hatuoni dalili zozote za kusaidiwa. Kuna hatari kubwa ya wengi kutokuwa na valid passports ifikapo 2015, Je tutawalaumu watu watapotumia njia za kienyeji na za vichochoroni kutatua tatizo lao?
  2. Kuna watu wameomba pasi imeshapita sasa miaka miwili na stakabadhi za malipo wanazo na wala hakuna jibu lolote la maana wanalopewa.
  3. Tuna watoto wetu waliozaliwa huku hawana pasi wanashindwa kusafiri na wazazi wao kuja Tanzania. Ubalozi unashindwa vipi kutoa huduma japo mara moja kwa mwaka?
Tunaamini udhalilishaji huu unatokana na filosofia ya Mh Balozi ya kutojali watu anaowaongoza maana inajulikana hata huko mikoani alipokuwa (Dodoma & Mwanza) wananchi hakuwa akiwajali. Tunahofia asije akawa anataka kuendeleza mfumo huo hata huku ughaibuni. Mbona Mheshimiwa Rais Kikwete yupo very simple? Anajali na huwatembelea raia wake mara kwa mara? Hata misiba ya raia wa kawaida huwa anahudhuria, sasa huyu Balozi yeye ni nani? Je yeye anajiona ni bora kuliko Rais wetu?

Tumelazimika kueleza yote haya si kwa sababu tunataka tu kulalamika LA HASHA, bali tumeona tukiendelea kuficha, kilio kitatuhusu. Yes KI - TA - TU - HU - SU.

Tunaviomba vyombo vyote vya habari vifikishe udhalilishaji huu kwenye idara husika hasa Bungeni na kwa Mheshimiwa Rais ili waelewe kuwa UBALOZI WETU WA ITALY HAUJALI WATANZANIA. UNAJALI MASLAHI YAO YA KIBINAFSI.

LABDA TAARIFA HII ITAZIAMSHA BALOZI NYINGINE ZIWEZE KUWAJALI RAIA WA TANZANIA. SISI TUNAJIVUNIA URAIA WETU HATA KAMA BALOZI HATUJALI NA TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAENDELEA KUIPENDA NA KUITUKUZA. TUTAFURAHI KUONA NA MABALOZI WETU WANAELEWA UMUHIMU WA KUWAJALI WATANZANIA KULIKO MASLAHI YAO YA KIBINAFSI.

Imeandikwa na :
(WAKEREKETWA WA UTURUKI, UGIRIKI, NA ITALY)

CREDIT: WANABIDII

No comments:

Post a Comment