Pages

Pages

Pages

Thursday 2 October 2014

SINGIDA WAJIANDAA KWA SERENGETI FIESTA


Baada ya kupagawisha wananchi wa Mbeya na shoo kali mwishoni mwa wiki iliyopita, tamasha la Serengeti Fiesta 2014 linaelekea Singida kukata kiu ya mashabiki wake ambao walikuwa wakilisubiri kwa hamu.
Shoo hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imepangwa kufanyika hapo Septemba 3, katika uwanja wa Namfua. Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake namba moja cha Serengeti Premium Lager ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo wamejipanga kutoa shoo bora kabisa kwa wananchi wa mkoa wa Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Chapa wa Kiwanda cha Serengeti Bwana Rugambo Rodney alidhibitisha uwepo wa wasanii watakaoporomosha shoo kali siku hiyo kuwa ni pamoja na Mwana Fa, Nikki II, Makomando, Stamina, Ney, Young Killa, Linah, Recho, Mr. Blue, Dully Sykes, Mo Music, Baraka Da Prince, Supa Nyotas:- (G-Luck, K-Style na Edo boy), “ Rodney aliendelea kusema kwamba....”Wakati ziara hiyo ikielekea ukingoni, ahadi yetu kwa mashabiki wetu wa Iringa ni kujiweka tayari kwa shoo kali hapo mjini kwao.”
Mwana Fa ambaye atatumbiza kwa mara ya kwanza katika shoo za tamasha la Serengeti Fiesta mjini Singida mwaka huu alisema....”Nimefarijika kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza mjini Singida na ningependa kuwashauri mashabiki wangu waje kwa wingi kunishuhudia jukwaani nikifanya mambo wakati wa shoo.”

Kabla ya shoo hiyo, kutakuwa na shughuli nyingine mbalimbali kama shindano la Serengeti Super Nyota Diva ambalo mshindi atajinyakulia tiketi kwenda kushuhudia shoo ya mwisho ya tamasha hilo litakayofanyika hapo Oktoba 18, 2014 jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment