Pages

Pages

Pages

Friday 24 October 2014

NIGERIA KUCHUNGUZA UTEKAJI MPYA WA WANAWAKE NA WASICHANA


Wanamgambo wa Boko Haram
Serikali nchini Nigeria inasema inachunguza taarifa ya idadi kubwa ya wanawake na wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na kwamba tangazo la kusitisha mapigano lililotolewa na majeshi ya serikali.

Msemaji wa Serikali ya Nigeria Mike Omeri, ameiambia BBC kuwa serikali ya Nigeria inajaribu kuthibitisha kile kilichotokea. Mwanakijiji mmoja anasema wanawake na wasichana arobaini wametekwa na kundi hilo.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitangazwa wiki iliyopita, lakini mashambulizi yanaendelea na mpaka sasa haijajulikana kama wasichana wa Chibok zaidi ya mia mbili waliotekwa na kundi la Boko Haram miezi sita iliyopita wataachiwa huru kama serikali ya Nigeria ilivyosema.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment