Pages

Pages

Pages

Thursday 23 October 2014

MNYIKA AWASILISHA MUSWADA BINAFSI WA BARAZA LA VIJANA

John Mnyika

Na Mary Geofrey
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amewasilisha muswada binafsi wa Baraza la Vijana la Taifa wa mwaka 2013 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

Aidha, muswada huo umeitwa mbele ya kamati hiyo ya kudumu ya bunge, kuendelea kusikiliza maoni ya wadau.

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa aarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, pamoja na kuendelea kupokea maoni ya wadau na kukutana na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo pia inaendelea kuujadili muswada huo.

Awali Mnyika akiwasilisha mswada huo, alisema anatarajia wabunge wa pande zote na vyama vyote kuunga mkono hoja ya  kuanzishwa kwa baraza hilo na kutumia madaraka yake kupitisha sheria hiyo katika mkutano wa 16 wa Bunge unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Kadhalika, Mnyika aliwataka wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, wadau na serikali kuzingatia kuwa  kwa zaidi ya miaka 18 ahadi za kukamilisha mchakato wa kuanzishwa kwa baraza  hazikutimia.

Alisema kuanzishwa kwa baraza hilo kutawezesha vijana kuanzia ngazi ya vijiji, mitaa hadi taifa, kuwa na vyombo vya kuwaunganisha vijana wa kike na kiume kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Alisema muswada huo unapaswa kupitiwa na Kamati ili uweze kusomwa kwa mara ya pili katika mkutano ujao wa Bunge kwa kuzingatia kuwa ni mikutano mitatu tu ya Bunge iliyobaki kabla ya kuvunjwa na kama  muswada huo usipopitishwa, Baraza litaundwa baada ya uchaguzi mkuu 2015.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment