Pages

Pages

Pages

Wednesday 1 October 2014

HIZI NDIZO NYARAKA 10 MUHIMU KUHUSIANA NA UCHOTWAJI WA MABILIONI YA ESCROW/IPTL

James Rugemalila (kushoto) Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engineering, na Harbinder Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited (PAP). Harbinder ni mzaliwa wa Iringa ('Mnyalukolo'), alikulia Iringa kabla ya kuzamia Kenya alikojenga urafiki na Gideon Moi, mtoto wa Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Toroitich arap Moi.

Harbinder Singh Sethi anatajwa kama mfanyabiashara wa Kenya na tajiri mkubwa, lakini alizaliwa na kulelewa Iringa, katika Nyanda za Juu Kusini. Katika umri wa miaka 20 na ziada kidogo, Sethi na kaka zake wawili Nota Singh na Manjit Singh walisajili kampuni ya Ruaha Concrete Co. Ltd (Novemba 1977), wote watatu wakitoa anuani ya S.L.P. 498 Iringa kama anuani yao. 


Katika miaka ya 1980, Singh alihamia Nairobi ambako alianza kuwa mbeba mifuko wa mwanae wa kwanza Rais Daniel arap Moi, Gideon. Anasemekana pia kuwa alikuwa rafiki wa karibu wa Nicholas Biwott, mwanasiasa na mfanyabiashara tajiri na mtu wa karibu wa Moi.

Akiwa nao anasemekana kumiliki sehemu ya mtambo ulioleta zogo wa megawati 47 wa Westmont mjini Mombasa, akiwa na Mukesh Gohil, Kamlesh Pattni, Bw. Gichuru, Mkurugenzi Mtendaji wa KPLC, Bw. Mutitu, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Gideon Moi (Oktoba 1997). 

Hivi karibuni, Sethi ameibuka na kuanza kutoa misaada mbalimbali kwa jamii kama sehemu ya uwajibikaji kijamii wa IPTL/PAP kwa kutoa michango kadhaa: Sh. 11milioni kwa SACCOS ya kundi la kwaya ya kanisani la Kanisa la Mtakatifu Rita Wakashia lililoko Kimara, Sh10 milioni kwa ujenzi wa kituo cha polisi cha Mbweni-Malindi, Sh14.5milioni kusaidia ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Petro jijini na Sh.20 milioni kwa ajili ya Chama cha Mchezo wa Riadha nchini (AT) kusaidia kufanyika kwa mashindano ya riadha ya taifa. (Jumla ya uchangiaji kwa uwajibikaji kijamii ni sh.55.5milioni). 

Kwa kificho pia, Sethi amekuwa akifadhili baadhi ya vyama vya siasa nchini ili kuhakikisha kwamba vinakaa kimya bila kuhoji uporaji uliofanyika. Uchunguzi wa kina wa matumizi ya vyama vyote vya siasa nchini ukifanyika kwa kulinganisha na ‘forensic investigation’ inayofanywa na TAKUKURU utaweza kuibua kiasi cha fedha ambacho Bw. Seth ametoa kwa vyama tajwa. Baadhi ya viongozi wa vyama hivi ni marafiki wa Seth wa muda mrefu.

Mfanyabiashara huyu ndiye anayehusika na uchotwaji wa mabilioni ya fedha za IPTL kupitia akaunti ya Escrow. Hizi hapa ndizo nyaraka muhimu kabisa zinazoelekeza mchakato wote na jinsi fedha zilivyochotwa kirahisi na kienyeji:


1-HUKUMU ILIYOIPA PAP IPTL BURE BIRASHI

2-MINITI ZA KIKAO BAINA YA IPTL NA TANESCO KUNDUCHI BEACH HOTEL 2013

3-IPTL BARUA YA MWANASHERIA MKUU KUHUSU KUCHOTWA KWA FEDHA

4-BARUA YA KATIBU MKUU ELIAKIM MASWI

5-BARUA YA 'MNYALUKOLO' KUKUBALI KUHUDHURIA KIKAO LAKINI AKIHIMIZA FEDHA ZIHAMISHWE HARAKA

6-MAPENDEKEZO YA SERIKALI KURUHUSU KUCHOTWA KWA FEDHA ZA ESCROW

7-KIAPO CHA FIDIA CHA IPTL

8-BARUA YA IPTL KUTAKA FEDHA ZILIPWE KUPITIA AKAUNTI YA PAP

9-HAYA NDIYO MAKUBALIANO YA KURUHUSU UCHOTWAJI WA FEDHA ZA ESCROW

10-BARUA YA MASWI KUTAKA BOT IRUHUSU FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW

No comments:

Post a Comment