Pages

Pages

Pages

Monday 27 October 2014

HAYA NDIYO MAKUBALIANO YA UKAWA

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa

MAKUBALIANO SABA YA UKAWA.
1. SERA,-Kudumisha sera za vyama vyote vinne na kuchukua mambo yanayofanana ili kuvifanya viwe na kauli ya Pamoja.
2.WAGOMBEA,-Kusimamisha wagombea wa pamoja katika chaguzi zote za Serikali za Mitaa, Wabunge, Baraza la Wawakilishi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar.
3.UTARATIBU,-Namna gani vyama vitashirikiana katika uchaguzi wa serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu na kusambaza Mwongozo katika mikoa mbalimbali kuwaelekeza viongozi mambo yanayotakiwa.
4.KURA YA HAPANA,-Kushirikiana katika mchakato wa kupiga kura ya hapana katika kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa kwa kuwa haijazingatia maoni ya Wananchi.
5.USHIRIKIANO,-Kufanya kazi kwa pamoja katika maswala ya msingi kwa maslah ya Nchi.
6.MUUNGANO,-Kuulinda muungano bila kuwa na migongano ya maslahi kama ilivyo sasa.
7.UZALENDO,-Kuhimiza na kusimamia ushirikiano wa pamoja baina yao na makundi mbalimbali bila kuweka mbele maslah yoyote ya vikundi na kuhakikisha Wananchi wanapata Tanzania mpya.

No comments:

Post a Comment