Pages

Pages

Pages

Wednesday 22 October 2014

FAMILIA YA REEVA YARIDHIKA NA HUKUMU YA PISTORIUS

Pistorius awaaga jamaa wake na familia akiondoka mahakamani kwenda kutumikia kifungo chake
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Pistorius aliondoka mahakamni na kupelekwa jela kwa gari la polisi
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
Jaji Masipa ametoa hukumu katika kesi ambayo imewagusa wengi kote duniani
Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.
Wazazi wa Reeva Steenkamp wameambia BBC kuwa walifurahia hukumu ya jaji na pia kuridhika kwamba kesi hiyo imekamilika.
Mwanariadha huyo wa kimataifa hataruhusiwa kukushiriki mashindano yoyote ya riadha kwa miaka 5 atakayokuwa jela hata ikiwa ataachiliwa kabla ya miaka hiyo kukamilika.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment