Pages

Pages

Pages

Thursday 25 September 2014

MSANII WA MAREKANI T.I KUTUMBUIZA FIESTA DAR

 Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ifraim Mafuru akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafala ya kumtangaza msanii wa Marekani TI ambaye atashiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Prime Time na meneja wa vipindi wa Radio Clouds FM Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika Dar es Salaam mwezi ujao.

 Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Allan Chonjo akizungunza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakimtangaza mwanamuziki TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Mkurugenzi Mkuu wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Efraim Mafuru (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Ruge Mutahaba katika hoteli ya Serena wakati wa kumtambulisha msanii TI wa Marekani ambaye atashiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
 

Mwanamuziki wa Kimarekani katika miondoka ya Hip-hop ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, mwigizaji na mwekezaji, Clifford Joseph Harris Jr, alimaarufu kama T.I. amethibitishwa rasmi na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd (SBL)kama mwanamuziki wa kimataifa atakayetumbuiza katika kilele cha shangwe za Serengeti Fiesta zitakazofanyika jijini Dar es salaam tarehe 18 Oktoba mwaka huu.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya SBL, Meneja Masoko Allan Chonjo alisema, " hivi karibuni tumetia saini na kukamilisha mikataba yote ili kuhakikisha kwamba mwanamuziki huyu wa kimarekani anafika Leaders Club jijini Dar essalaam tarehe husika"
Chonjo aliendelea kusema, 'Tungependa kuwashukuru washirika wetu, Prime Time Promotions kwa kuhakikisha tunakamilisha mikataba yote na vile vile kwa kuhakikisha kamba tamaha hili linakamilika kwa mafanikio. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwamba T.I kutia mguu wake katika ardhi ya Tanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari, Sebastian Maganga kutoka Prime Time Promotions, alikuwa na haya ya kusema, "kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa tukihakikisha kwamba tunaelewa nini watanzania wanataka na tumekuwa tukijitahidi bila kuchoka kuhakikisha kamba tukio tunalolifanya, kwa mwaka huu, wapenzi wetu watashuhudia shoo ya nguvu ambayo haijawahi yanyika hapa nchini.
"Mpaka sasa, Serengeti imetembelea mikoa kumi (10) nchini, na itaendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Singida, Songea, Mtwara, Dodoma na Mbeya.
Katika mabadiliko mengine Serengeti Breweries na Prime Time Promotions wamewaomba mashabikiwachague msanii wa kitanzania ambaye wangependa atumbuize na TI. “Hiki ni kitu kipya natunataka kuhakikisha kwamba mashabiki wanaburudika vya kutosha, alisema Maganga. ‘Habari zitasambazwa kwa njia ya TV na redio kuelezea jinsi ya kushiriki’, aliongeza.
Serengeti Fiesta inatambulika kwa kuleta wasanii wa kimataifa hapa nchini, miongoni mwao ni pamoja na Rick Ross, Shaggy na Davido
T.I aliyetamba na kibao "No Mediocre" amekuwa akijishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo biashara. Yeye ni muasisi na mkurugenzi mkuu wa Grand Hustle Records.
T.I. alianza kupata umaarufu mwaka 2003, baada ya kushirikishwa na  mwanamuziki mwenzake Bone Crusher, ambaye ni mkazi wa  Atlanta,  katika wimbo wa  "Never Scared". Alipata umaarufu zaidi baada ya kutoa wimbo wa Trap Muzik (2003).
Mwaka 2004, T.I. alionekana kwenye wimbo wa Destiny's Child's "Soldier", sambamba na Lil Wayne. Albamu ya sita ya TI, Paper Trail (2008), ilikuwa albamu yake ya mafanikio zaidi , na imefanikiwa kuuza nakala 568,000 katika wiki ya kwanza nchini Marekani na kuifanya ya tatu katika chati ya albam bora nchini humo. Mpaka sasa, T.I. amdeshinda tuzo tatu za Grammy Awards.
T.I. pia ametoa nyimbo kama vile"Bring Em Out", "What You Know", "Swagga Like Us" (akimshirikisha Kanye West, Jay-Z and Lil Wayne), "Dead and Gone" (akimshirikisha Justin Timberlake), "Ball" (akimshirikisha Lil Wayne) and "No Mediocre" (akimshirikisha Iggy Azalea).

No comments:

Post a Comment