Pages

Pages

Pages

Sunday 21 September 2014

MKURUGENZI WA TIGO NYANDA ZA JUU KUSINI ATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA WATUMIAJI MAJI KATA YA NZIHI, IRINGA VIJIJINI

Mkurugenzi wa Nyanda za Juu Kusini wa Kampuni ya Tigo, Jackson Kiswaga akikabidhi msaadaa wa pikipiki kwa Jumuiya ya watumiaji maji kata ya Nzihi, Iringa vijijini; anayepokea ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Damas Kitinye.
Hapa akimkabidhi kadi ya pikipiki hiyo itakayofanya kazi ya kufuatilia huduma za usambazaji maji katika kata hiyo
Baadhi ya watendaji wa vijiji vya kata hiyo waliohudhuria hafla hiyo.
MKURUGENZI wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Kampuni ya Simu ya mkononi ya Tigo, Jackson Kiswaga amemaliza kero ya usafiri iliyokuwa ikiikabili Jumuiya ya Watumiaji Maji Kata ya Nzihi, Iringa vijijini baada ya kuwapa msaada wa pikipiki waliokuwa wakihitaji kwa muda mrefu.
Makabidhiano ya pikipiki hiyo yalifanywa juzi katika hafla fupi iliyoshirikisha wenyeviti wa vijiji vya kata hiyo, viongozi wa kata, halmashauari na baadhi ya watumiaji maji.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Steven Mhapa alisema; “tulipeleka maombi kwa wadau mbalimbali wa maendeleo wa halmashauri hii, tukiomba msaada wa pikipiki kwa ajili ya matumizi ya jumuiya hiyo. Mmoja kati yao ambaye ni Bwana Kiswaga hakusita kutusaidia.”
Akishukuru kwa msaada huo, Mhapa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nzihi alisema chombo hicho cha usafiri kitaiwezesha jumuiya hiyo kusafiri eneo moja hadi lingine kufuatilia maendeleo na changamoto zinazoukabili mradi wa maji katika kata hiyo.
Meneja wa Watumiaji Maji wa Kata hiyo, Hamza Chorobi alisema mradi wa maji katika kata hiyo unazo changamoto zingine na akazitaja kuwa ni pamoja na uchakavu wa miundombinu yake na ongnezeko la watumiaji wa huduma hiyo.
Alisema ili uweze kukidhi mahitaji ya kata hiyo kwasasa, mradi huo wa maji uliojengwa mwaka 1986 na kuanza kutumika 1999 unahitaji zaidi ya Sh Milioni 300 za ukarabati wa miundombinu yake.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alimuomba Kiswaga kutumia ujirani alionao na wawekezaji kuwaomba waangalie uwezekano wa kuisaidioa serikali na wananchi wa kata hiyo kukabiliana na changamoto hiyo.
Akikabidhi msaada huo Kiswaga alisema; “mimi ni mwenyeji na mzaliwa wa mkoa wa Iringa, ninaguswa sana na matatizo ya ndugu zangu. Ninapopata nafasi ya kusaidia huwa nafanya hivyo, sio hapa Nzihi pekee ambako nimezaliwa lakini katika maendeleo sehemu mbalimbali za mkoa wa Iringa.”
Alisema Utekelezaji wa Ilani ya CCM unahitaji nguvu ya serikali na wadau wake wote wa maendeleo kwa kuzingatia kwamba hakuna serikali duniani kote iliyoweza kufanya mambo yake bila msaada wa watu na wadau wake.
Alisema kila anapopata fursa ya kukutana na watu wa ndani na nje ya nchi wanaoweza kusaidia maendeleo ya watu wengine amekuwa akiyakumbuka matatizo ya watu wa Iringa na kuwaomba.
“Nimekutana na wadau Marekeni, Ulaya na Afrika Kusini kuna mambo yanakuja katika sekta ya afya na elimu na yatakapokuwa tayari nitawaleta watu hao,” alisema.
Kwa upande wao wenyeviti wa vijiji vya kata hiyo walimpongeza Kiswaga kwa msaada huo huku wakiwataka wadau wengine wajitokeze kusaidia maendeleo ya wananchi.

No comments:

Post a Comment