Pages

Pages

Pages

Thursday 4 September 2014

KIKAO CHA NATO CHAITUHUMU URUSI



Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen
Viongozi wa nchi za Magharibi wameishutumu Urusi kwa "ushawishi" wake katika mgogoro wa Ukraine, mwanzoni mwa mkutano wa viongozi wa Nato huko Wales, Uingereza.
Nato na Uingereza zimeonya kuwa shinikizo juu ya Urusi litaongezeka iwapo haitabadili msimamo wake kuhusu eneo la mashariki mwa Ukraine.
Watu wapatao 2,600 wamekufa katika vita kati ya majeshi ya Ukraine na waasi.Rais wa Ukraine atawapa taarifa viongozi wa Marekani na Ulaya kuhusu mazungumzo ya awali kati yake na Rais Vladmiri Putin wa Urusi juu ya mpango wa kusitisha mapigano nchini Ukraine.
Nchi za magharibi zinasema zina ushahidi kwamba Bwana Putin anawaunga mkono wapianzani wanaotaka kujitenga kutoka Ukraine kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi na silaha, lakini Urusi inakana tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuyakimbia makaazi yao mashariki mwa Ukraine.
Mkutano huo wa siku mbili mjini Newport utatawaliwa na mjadala kuhusu mgogoro wa Ukraine.
Viongozi hao wanatarajia kutoa mapendekezo yao ya pamoja kuhusu masuala yanayohusu makundi yenye itikadi kali za kiislam nchini Iraq.
Rais Obama amekuwa akijaribu kupata uungwaji mkono kutoka kwa mataifa haya kwa ajili ya kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo wa Islamic State, kundi ambalo analiita mwenyewe Saratani ambayo lazima iondoshwe kutoka eneo la Mashariki ya kati.
Kikao cha viongozi wa Nato, Wales, Uingereza
Dennis Ross, ambaye alikuwa msaidizi maalum wa rais Obama kuanzia mwaka 2009 hadi 2011, amesema lazima kuwe na lengo kwa Syria na pia Iraq.
Viongozi hao wa NATO wanatarajiwa kukutana na rais wa Ukraine Petro Poroshenko, ili kuimarisha ushirikiano wa wanachama wa kundi hilo.
Mazungumzo hayo yanakuja baada ya mkutano wa upatanishi Mashariki mwa Ukraine.
Mwandishi wa BBC kuhusu maswala ya ulinzi, anasema kuwa bwana Poroshenko amealikwa kwa mkutano huo kama ishara ya umoja.

Viongozi wa NATO watakuwa wanajadili tatizo na tisho linalotokana na kundi la Islamic State. Rais Obama na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, wametoa wito jitihada za pamoja dhidi ya makundi yenye itikadi kali za kiisilamu nchini Syria.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment