Leo kuanzia saa tano Asbh Mkurugenzi wa PCC amekutana na CAG kama hatua ya mwisho ya kubadilishana taarifa za kiukaguzi na kiuchunguzi kuhusu tuhuma za ukwapuaji wa billion 200 ndani ya akaunti ya escrow bank kuu. Kwa mujibu wa taarifa za ndani taasisi zote mbili zinahitimisha kazi zao wiki hii.
Kwa mujibu wa taratibu CAG atakabidhi taarifa yake kwa Waziri mkuu na Kwa Bunge kwa mujibu wa utaratibu na taarifa hiyo itapaswa kuwa wazi kwa mjadala ingawa mpaka sasa taarifa ndani ya ofisi ya katibu wa bunge zinaonesha kuna mkakati wa kuzuia report hiyo isipangwe kujadiliwa bunge lijalo kutokana na hofu ya madudu yaliyomo kwenye report hiyo ya CAG. Kwa upande wa report ya pccb Dr Hosea atawajibika kuikabidhi taarifa hiyo kwa waziri Mkuu sambamba na DPP tayari kwa mashtaka kwa makosa yatakayobainika ya kimahakama.
Mambo makubwa katika uchunguzi huu ni; kwanza uhalali wa singasinga kupewa 200bn za escrow na pili uhalali wa singasinga kumiliki IPTL..
Katika hali inayotazamwa kama dalili za kuchukuliwa mamuzi magumu kuhusu ufisadi huu, baada ya JK kutoka US kwenye mkutano na Obama ambapo habari zilivuja kuhusu hoja ya ufisadi kama kigezo cha Tanzania kupata msaada wa MCC2, siku moja baada ya JK kuwasili nchini alimwondoa kwenye nafasi ya u DPP Mhe Felishi pamoja na Mhe Lilian aliyekuwa mkurugenzi wa uchunguzi PCCB chini ya Hosea.
Wote wawili waliteuliwa kuwa majaji. Wawili hao wamekuwa kikwazo kwa Dr Hosea kwa muda mrefu na kumekuwa na mnyukano wa ndani ulivuka hata vyombo vya habari. Report ya PCCB na CAG ni muhimu sana kwani mpaka sasa nchi wahisani hakuna iliotoa msaada wa kibajeti tangu bajeti ipitishwe mpaka sasa zote zikisubiri report hizi na kuona hatua ambazo serikali itachukua.
Aidha Obama alimwambia JK kuwa mradi wa MCC2 inasainiwa sept 2014 hivyo namna serikali itakavoshughulikia uchafu huu ni kipimo cha kama inastahili kupata au kukosa kwani kigezo cha fedha za MCC ni uwajibikaji katika vita dhidi ya rushwa.
Swali la msingi na hamu kubwa ni kuona ni kwa kiasi gani report hizi mbili zitahitimisha mwendelezo huu wa ufisadi kupitia IPTL ambao umekuwepo tangu awamu ya pili na sasa awamu hii umebebwa na kutetewa na hata na Waziri Muhongo na Maswi kwa nguvu zote huku Werema akitamani kuchukua sheria mkononi kukata kichwa cha Mbunge.