Pages

Pages

Pages

Tuesday 23 September 2014

HATMA YA QATAR NA KOMBE LA DUNIA 2022 BADO KITENDAWILI

Mohamed bin Hammam, Makamu wa Rais wa Fifa aliyejiuzulu

Ripoti iliyotolewa kuhusu tenda ya kuhodhi michuano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 na mwaka 2022 imeelezwa huenda ikasabisha wanaoshutumiwa kufunguliwa mashtaka
Mbunge wa Chama cha Conservative nchini Uingereza, Damian Collins aliitaka ofisi inayochunguza maswala ya udanganyifu na rushwa
kuomba nakala ya ripoti iliyotolewa kuhusu mchakato wa kutoa tenda kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022, akisema kuwa anaamini Ripoti hiyo huenda inatoa ushahidi kuhusu madai ya vitendo vya rushwa.
Mwanasheria kutoka nchini Marekani, Michael Garcia alitoa ripoti yake mwezi huu, lakini Fifa imesema yaliyomo kwenye ripoti hiyo hayatatolewa hadharani.
Kamati ya Qatar iliyokuwa ikiwania tenda kuhodhi michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 inakabiliwa na shutuma kuwa ilitoa rushwa kupatiwa nafasi hiyo,baada ya Gazeti moja kuripoti mwezi juni kuwa aliyekuwa makamu wa rais wa fifa Mohamed bin Hammam alitoa rushwa ya pauni milioni tatu ili kupata tenda hiyo.madai ambayo Qatar imeyakanusha.
Uamuzi baada ya kutoka kwa ripoti hiyo utatolewa mwakani.
BBC/MICHEZO

No comments:

Post a Comment