Pages

Pages

Pages

Sunday 3 August 2014

ZAIDI YA WATU 150 WAUAWA KATIKA TETEMEKO CHINA

Mtoto aliyejeruhiwa kwenye tetemeko la Yunnan, Uchina

Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa eneo la kusini-magharibi mwa Uchina.
Vyombo vya habari vya Uchina vinasema kuwa watu kama 150 wameuawa na wengi kujeruhiwa.
Wakuu wa huko wanasema majengo mengi yameangamia,pamoja na nyumba na shule na mawasiliano yameathirika sana.Shirika la Marekani linalochunguza ardhi linasema kitovu cha tetemeko hilo la kipimo cha 6.1 kilikuwa kwenye eneo la mbali la milima katika jimbo la Yunnan.
Watu walihisi tetemeko hilo piya katika majimbo ya jirani ya Guizhou na Sichuan.
Eneo la kusini-magharibi la Uchina liko katika kanda inayotingishwa mara kadha na mitetemeko.
Tetemeko lilotokea Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu maelfu kadha.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment