Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 9 August 2014

WANAMITINDO WAGEUKIA MITANDAO YA KIJAMII KUJINADI

Wabunifu wakomavu na chipukizi wanaonyesha mitindo yao katika maonyesho ya mitindo ya kiafrika mjini London wiki hii.
Lakini katika enzi ambapo wanablogu wa mitindo wanaotumia video kuonyesha mitindo yao, mwandishi wa BBC Alexis Akwagyiram anatathmini ikiwa darubini imehamishwa kutoka kumbi za maonyesho hadi katika mitandao ya kijamii.
Maonyesho kama hayo ndio yanayoshuhudiwa katika maonyeso ya kila mwaka mjini London hii ikiwa mara yake ya nne.Ulingo wa fasheni umejaa picha za wanamitindo warembo wanaotembea katika kumbi za fasheni wakiwa wamevalia nguo za kupendeza zenye mitindo mbali mbali.
"Afrika kwa sasa inang'aa," asema Josette Matomby, msimamizi wa maonyesho kutoka DRC ambae pia ni mbunifu anayeishi London. Yeye pia ni mmoja wa waasisi wa maonyesho haya ya London.
Anataja kampuni ya Vlisco ya uholanzi kama moja ya kampuni zenye kueneza mitindo ya kiafrika.
Bi Matomby anasema nguo za kiafrika zimeanza kuwika katika ulingo wa kimataifa katika miaka ya hivi karibuni na hata kuvutia kampuni kubwa za mitindo kama vile Burberry.
Hofu kwamba, wabunifu wa kiafrika hawakuwa wakifaidi kutokana na kazi zao ilikua sehemu ya msukumo wao wa kuanzisha maonyesho kama haya ya kupigia debe mitindo yao Afrika na ughaibuni.
'Mitandao ya kijamii'
Wateja wakongwe hependa wakati mwingine kuvishwa na kurembeshwa na wataalamu
Mitindo mingi ambayo huvaliwa Afrika hutengezwa nchini Uholanzi.
"tunapaswa kutengeza vitambaa vya hali ya juu sisi wenyewe. Nataka waafrika wawe wawekezaji katika wao wenyewe, '' asema Bi Matomby.
Lakini kinachodhihirika wazi, ni kwamba kuna waraibu wengine wa mitindo ambao siku hizi wanapatikana katika mitandao ya kijamii kama vile YouTube, Instagram na Twitter, pamoja na blogu.
Waraibu hawa wa mitindo wanaitumia mitandao hiyo kuonyesha ubunifu wao na pia kuibua mitindo zaidi mipya.
Kwa kufanya hivyo wanawaleta wanamitindo wa Afrika pamoja na wanamitindo wa kimataifa.
Shirley B Eniang ni kijna anayependa mitindo na anaonyesha hilo kwa kutumia video anazozionyesha kupitia kwa blogu.
Ana asili ya Ghana na Nigeria ingawa anaishi London. Yeye huwaonyesha zaidi ya watu nusu milioni mitindo tofauti kupitia mtandao wa kijamii wa You Tube. Video zake zimetazamwa na zaidi ya watu milioni kumi kwenye akaunti yake. Mtindo huu unajulikana kama 'Vlogging'
Mbunifu mwingine Oghosa Ovienrioba, mwenye umri wa miaka 22 mzaliwa wa Uingereza ingawa ana asili ya Nigeria, ana akaunti ya You Tube na akaunti yake ina mashabiki 10,000.
Mitandao ya kijamii imewaweka wabunifu wa mitindo ya Afrika katika ulingo tofauti wa kimataifa
'Ulingo wa kimataifa'
Lupita Nyong'o ameonekana kurejesha muonekano mzuri wa kimataifa kwa sura ya Kiafrika
Mitandao ya kijamii bila shaka imewasaidia wabunifu wa Afrika kujulikana na kusifika katika maonyesho ya kimataifa ya mitindo , wengi wanaona hili kuwa demokrasia katika sekta ya mitindo.
Mitindo ya kiafrika zamani ilionekana kama ya waafrika pekee lakini mtu yeyote mwenye tamaa ya kupata mitindo ya kiafrika anaweza kuipata kwa njia yoyote, njia kuu ikiwa kupitia hiyo mitandao ya kijamii ikilinganishwa na siku za nyuma.
Katika siku za usoni, itakuwa muhimu na lazima kwa wabunifu wa mitindo kuwa na akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii kuweza kuionyesha kwa dunia nzima na pia ili kuweza kupata wateja.
Bado kuna nafasi kwa maonyesho ya mitindo ya Afrika , bado kuna nafasi hiyo kwa sababu hii inawapa nafasi wabunifu kuonyesha mitindo yao kwa kuwavalisha wanamitindo nguo na vitambaa vyenye mvuto na hata kuwafunza watu namna ya kuvalia nguo hizo.
Lakini kutakuwa na wakati, ambapo kutakuwa na maonyesho mengi ya mitindo ya kiafrika.

Maonyesho hayo pia hufanyika mjini Berlin na New York, na hata katika sehemu zingine katika bara la Afrika.
BBC/SWAHILI-MAKALA

No comments:

Post a Comment