Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 18 August 2014

WALIOKIMBIA ZAHANATI YA EBOLA WATAFUTWA

Ebola  Liberia
Kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine. Kituo kiko kwenye mtaa wa West Point, wenye wakazi wengi.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment