Pages

Pages

Pages

Monday 18 August 2014

WAKURDI WASHIKILIA BWAWA MUHIMU IRAQ

Bwawa muhimu la uzalishaji wa umeme linaloshikiliwa na Wakurdi

Chanzo cha habari cha Kikurdi kimeiambia BBC kwamba wapiganaji wake wa Peshmerga wameliweka katika himaya yao bwawa muhimu lililopo kaskazini mwa Iraq kutoka mikononi mwa wapiganaji wa kiislamu, huku ikulu ya Marekani ikisema kuwa mashambulizi ya ndege zake katika eneo hilo hayatakoma kwa kuwa zinalinda maslahi yake nchini humo. Baruan Muhuza ameandaa taarifa Zaidi.
Chanzo hicho kimesema kuwa Wanajeshi wa Kikurdi wanajaribu kusafisha eneo lenye madini na mabomu ya kutegwa ambayo yameachwa mahala hapo na kikundi cha wapiganaji wa himaya ya kiislamu. Mashambulizi yao ya chini ya ardhi yamekuwa yakiunganishwa na msaada wa vikosi vya askari wa Marekani ambao wanatoa ulinzi wa anga.
Usiku wa kuamkia leo Ikulu ya Marekani imesema itaendelea na mashambulizi ya anga kama ilivyoamuriwa na Rais wa nchi hiyo Barack Obama, ikiwa ni mkakati wa sera ya Marekani ya kulinda watu na mali zake zilizopo Iraq.Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Marekani imesema makundi kumi na nne ya wanamgambo hao yametimuliwa mchan wa jumapili na ndege za kivita za Marekani zikiwemo zile zisizo na rubani.
Maafisa wa White House wamesema bwawa lililo kombolewa ni muhimu kwa maji na umeme na kwamba endapo lingeachwa kwa wanamgambo hao na kulifumua kingo zake lingesababisha mafuriko kwenye mji wa Mosul na pengine hadi jijini Baghdad mahala ambapo kuna ubalozi wa Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa Iraq anayeondoka madarakani Hoshyar Zebari ameiambia BBC Mjini Baghdad kuwa wapiganaji wa himaya ya kiislamu wameleta changamoto kubwa kwa Iraq na kwamba ni tishio kwa dunia.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment